Mratibu wa Kamati ya Jukwaa la Utawala wa Mtandao (IGF) Nazar Nicholas akifafanua jambo wakati wa kikao cha wadau wa mtandao waliokutana jijini Arusha leo Oktoba 16,2019 kujadilia mafanikio na changamoto katika mtandao

 Mtaalamu wa lugha ya alama (aliyekaa katikati) akiendelea kutoa tafsiri ya kinachojadiliwa kwa watu wenye uhitaji maalumu wakiwemo wenye ulemavu ambao wameshiriki katika kongamano hilo ambalo limewakutanisha wadau kujadili masuala ya mtandao .

Mtalaamu wa masuala ya Intanet ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo cha Uhasibu Arusha(IAA)Profesa Eliaman Sedoyeka akizungumza mbele ya washiriki wa kongamano la kujadili masuala ya mtandao ambalo limendaliwa na Jukwaa la Utawala wa Mtandao(IGF).
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada ambazo zinaendelea kujadiliwa katika kongamano la masuala la matumizi ya mtandao.Kongamano hilo linaendelea jijini Arusha ambalo limeanza leo 


Na Said Mwishehe, Arusha 

JUKWAA la Utawala wa Mtandao Tanzania (IGF), limewakutanisha wadau, taasisi za Serikali na asasi mbalimbali za kiraia kujadili mafanikio na changamoto zinazotokana na matumizi ya mtandao huku wanawake wakitajwa kuongoza katika matumizi ya mtandao biashara mara mbili Zaidi ya wanaume duniani. 

Akizungumza leo Oktoba 16,2019 katika ufunguzi wa kongamano hilo linaloendelea jijini Arusha, Mtaalam wa masuala ya mtandao na mkufunzi katika chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Profesa Eliamani Sedoyeka amesema kasi ya matumizi ya biashara mtandao imekuwa kubwa sana katika miaka ya karibuni tofauti na hapo awali. 

Amesema katika utafiti alioufanya mwaka jana nchini, aliweza kugundua kuwa wanawake wamekuwa wakitumia fursa za uwepo wa mitandao katika kutangaza, kununua na kuuza kwa njia ya mitandao mara mbili Zaidi ya wanaume. 

Profesa Sedoyeka kupitia kongamano hilo ametoa mwito kuwataka watumiaji wa mitandao kuitumia katika njia salama ili kuepuka kutapeliwa hususani kwa wanaotumia kwa ajili ya kufanya biashara. 

Hata hivyo amesema mtandao kama rasilimali muhimu bado haitumiki vizuri kwani kuna tatizo la baadhi ya watumiaji kutoamini kama njia sahihi ya kufikisha ujumbe na ndio maana baadhi ya watu wakitumiwa barua kwa njia ya mtandao lazima watapiga simu kwaajili ya kuhakiki. 

Amewataka watumiaji wa mtandao kuweka nywila (password), ili kuepuka watu wanaotumia vibaya mitandao kwa kufanya uhalifu na kwamba endapo utapenda kumpatia mwenza wao nywila hiyo lakini lazima kuhakikisha simu au kompyuta imewekwa nywila. 

Kwa upande wake Mratibu wa Kamati ya Jukwaa la utawala mtandao Tanzania, Nazar Nicholaus, amesema matumizi ya mtandao yamekuwa na changamoto kubwa sana ambapo watu wamekuwa wakiitumia vibaya bila kujua athari za baadae. 

“Tumekuwa tukifuatilia yanayoendelea mtandaoni, bado kuna baadhi ya watu wanaitumia vibaya na wengine kutoa taarifa ambazo si sahihi.Kwa mfano hivi karibuni kuna mtu aliamua kutumia mtandao kutoa taarifa za kwamba mmoja ya Waziri Mkuu mstaafu nchini (akamtaja) amefariki dunia wakati sio kweli.Kuna mifano mingi tu ya matumizi yasiyo sahihi. 

“Ni jukumu la kila moja wetu kuhakikisha tunaitumia mitandao vizuri na ukweli uliopo katika mitandao kuna mambo mengi yenye tija Zaidi kwa maendeleoe ya nchi yetu.Mtandao ni zakidi ya kutuma picha katika Whtsap na facebook, hiyo ni sehemu ndogo sana na tunaweza kusema kama ni asilimia basi ni 0.0001,”amesema Nicholas. 

Kuhusu kongamano ambalo limewakutanisha wadau hao Nicholas amesema IGF inatambua umuhimu wa kuwakutanisha wadau wa masuala ya mtandao kwa ajili kukaa pamoja kujadiliana na kubadilisha mawazo kuhusu njia bora ya kutumia mtandao na hivyo anaamini kupityoia kongamano hilo watatoka na mawazo yaliyo bora. 

“IGF tutaendelea kuwakutanisha wadau wa mtandao kwa ajili ya kujadiliana kwa pamoja.Tulikuwa tumesinzia kidogo lakini sasa tumeamka na binafsi niliamua kuchukua jukumu la kuhakikisha wadau wanakutana.
amesema Nicholas. 

Kuhusu nafasi ya watu wenye mahitaji maalumu wakiwamo wenye ulemavu kushirikishwa katika IGF, Nicholas amesema kwa kutambua nafasi yao imekuwa ikiwashirikisha na hata kwenye kongamano linaloendelea wameshirikishwa kikamilifu na mawazo na maoni yao yatapewa kipaumbele.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...