Mkurugenzi Mkazi wa kampuni ya Addscoin Tanzania Japhet Birunda akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mikocheni jijini Dar es salaam wakati alipoelezea uzinduzi wa Sarafu ya Kidigitali utakaofanyika Oktoba 26,2019.
Mhandisi na mtaalamu wa Block Chain na Capital Currency Bw. Richard Charles  akizungumza namna Sarafu hiyo ya kidigitali inavyoweza kufanya kazi.
Japhet Birunda Mkurugenzi Mkazi wa kampuni ya Addscoin Tanzania na Fred Mushi Katibu Mtendaji wa Kamuni ya Addscoin Tanzania Ltd na maafisa wengine wakiwa kwenye mkutano huo.

..................................................

Kampuni ya Addscoin Tanzania Ltd imeanzisha mradi wa kutoa huduma ya elimu juu ya tekinologia mpya ya Block Chain unaosafirisha fedha kwa njia ya Mtandao katika kuendeleza uchumi wa viwanda ambapo pia inahamasisha watu kuwekeza kwenye mradi wa IRA (Insetive Research Africa) ambapo malipo yake yanatumia sarafu Diligence ya kidigitali . 

Hayo yamesemwa na Japhet Birunda Mkurugenzi Mkazi wa kampuni ya Addscoin Tanzania wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za kamppuni hiyo zilizopo Mikocheni jijini Dar es salaam.

Amesema kampuni ya Addscoin Tanzania Ltd imeunda mfumo wa kusaidia kutunza sarafu za Kidigitali Bitcoin , Ethelium, na Diligence ambazoo zitatumiwa na watanzania wanaotumia msaada wa Block Chain kusafirisha na kutunza fedha. pia mfumo huu utasaidia serikali kujua kiwango cha pesa zinazotunzwa na watanzania kwenye Sarafu Digitali.

Bw. Japhet ameongeza kuwa Kampuni hiyo iko katika mazungumza na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kama msimamizi mkuu wa taasisi za kifedha ili kuona namna itakavyoweza kufanya kazi na kutekeleza majukumu yake hapa nchini. 

Ameongeza kuwa Oktoba 26 .2019 kwenye hoteli ya Akemi jijini Dar es salaam kampuni hiyo pia itazinduwa kampeni ya mfuko wa utunzaji mazingira duniani “Green Care for Future Life” utakaochangiwa na mataifa yote duniani kwa msaada wa Tekinolojia ya Block Chain na sarafu Digitali sambamba na uzinduzi wa Exchanger Platform Wallet iitwayo “Sell Bitcoin 

Japhet amesema kwa kushirikiana na taasisi ya kijamii inayoratibu mazingira Tanzania (WETAAIFICO watahamasisha jamii kushiriki katika utunzaji wa mazingira duniani pote kwa msaada wa (Block chain). 

Uzinduzi huo utaambatana na mkutano mkubwa utakaojumuisha wadau wote wa maendeleo ya kiuchumi kutoka sekta zote nchini ili kutambua fursa kwa wawekezaji na kutambua tekinolojia mpya ya kuwekeza na kupata faida maradufu ya kidijitali.

Kwa heshima na taadhima tunawaalika kufanya mawasiliano ili kupewa utatibu mzuri zaidi wa namna ya kuhudhuria mkutano huo bila kukosa. tayari nafasi zimechukuliwa na zilizobaki ni chache tu. 

Kampuni Addscoin Tanzania Ltd imesajiliwa kisheria kwa usajili Namba 139341325 kutangaza na kuuza pamoja na kuendesha (Block Chain Technolog na Sarafu Digitali) na ina vibali vya kuendesha biashara hiyo kisheria kutoka Brela ili kubuni miradi ya kibiashara kwa msaada wa Block Chain inayoweka mazingira kwa washiriki wote kulipa kodi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...