Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Faraji Mnyepe akizungumzia maadhimisho ya miaka 74 ya Umoja wa Mataifa yatakayofanyika Kitaifa kesho jijini Dodoma.
Kaimu Mratibu wa Umoja wa Mataifa, Michael Dunford akizungumza na wandishi wa habari kuelezea siku ya Umoja wa Mataifa ambapo hufanyika kila Oktoba 24 ya kila mwaka. Kesho Umoja huo unatimiza miaka 74 tangu kuanzishwa kwake.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (kulia) akizungumza jambo na Kaimi Mratibu wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Michael Dunford wakati wa mkutano wao na wandishi wa habari kuelezea maadhimisho ya miaka 74 ya UN yatakayofanyika kesho.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Faraji Mnyepe akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa umoja wa mataifa (UN)



Charles James, Michuzi TV

Kuelekea maadhimisho ya miaka 74 ya Umoja wa Mataifa (UN), Tanzania imesema imepiga hatua kubwa katika suala la usawa kwenye jinsia kwa kutoa kipaumbele wa nafasi za uongozi kwa wanawake.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Faraji Mnyepe alipokua akizungumzia maadhimisho hayo ambayo kitaifa yatafanyika jijini Dodoma.

Dk Mnyepe amesema maadhimisho hayo yenye kauli mbiu ya Wanawake na Wasichana kuwa kipaumbele kufikia malengo ya Dunia ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof Palamagamba Kabudi.

" Tunashukuru ushirikiano ambao tunaoneshwa na ndugu zetu wa UN hasa katika kutoa elimu juu ya nafasi ya mwanamke katika uongozi. Tunaomba wananachi wa Dodoma kujitokeza kwa wingi kesho katika viwanja vya Nyerere ambapo itakua mara ya kwanza kwa maadhimisho haya kufanyika jijini hapa.

Kama Taifa tumekua mstari wa mbele kupigania haki ya mtoto wa kike na wanawake kwa ujumla. Tunaamini katika usawa hivyo nitoe rai kwa watanzania kuendelea kuwaamini wanawake katika mambo mbalimbali kielimu, kisiasa, kitamaduni na hata kiuchumi," Amesema Dk Mnyepe.

Amesema licha ya Prof Kabudi kuwa mgeni rasmi sherehe hizo zinatarajiwa pia kuhudhuriwa na mabalozi wa nchi mbalimbali, mashirika ya kimataifa, viongozi wa serikali na waakilishi wa makundi mbalimbali likwemo la wenye mahitaji maalumu.  

Akizungumza kwa niaba ya Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini, Balozi Michael Dunford amesema sherehe hizo zimelenga kuhimiza usawa wa kijinsi huku akiipongeza Tanzania kwa kupiga hatua katika utekelezaji wa lengo namba 5 la malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) ambalo linazunguzia usawa wa kijinsia.

 “ Tunaamini kama nchi itafanikiwa katika lengo la usawa wa kijinsia basi malengo yote ya maendeleo endelevu yatafanikiwa. Kwa upande wa Tanzania imepiga hatua katika lengo hili katika sekta mbalimbali zikiwemo elimu na afya, hivyo sisi kama Umoja wa Mataifa tutashirikiana na serikali katika kufikia lengo hili.”

Umoja wa Mataifa umekua ukifanya maadhimisho haya kila ifikapo Oktoba 24 ya kila mwaka ambapo mwaka huu yatafanyika jijini Dodoma na kushuhudiwa gwaride maalumu la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na bendera ya UN itapandishwa kwa mara ya kwanza Dodoma ikiwa ni Makao Makuu ya Nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...