Kamishna Mhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)Profesa Dos Santos Silayo akiongea na Global Education Link TV,kuhusu Tuzo za Taaluma katika Sekta ya Elimu nchini.

TFS ni mmoja wa wadhamini wa tuzo hizi zilizoandaliwa  (TAMISEMI) kwa kushirikiana na Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA),ambazo kwa pamoja  zinategemewa kuleta  matokeo makubwa katika sekta ya elimu nchini.

Profesa Silayo amependekeza kuwa,ndani ya tuzo  hizo katika kioengele  cha ubunifu, kuwepo na shule bora katika uhifadhi wa mazingira ili kutoa fursa kwa wanafunzi kujifunza masomo yanayohusiana na masuala ya misitu na nyuki.

Mbali na hilo ametoa ushauri kwa mashirika binafsi,taasisi za Serikali na watu binafsi kushirikiana katika kuinua elimu kwa kutoa kipaumbele na motisha katika sekta ya elimu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...