Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
SHIRIKA la Umeme nchini (Tanesco) Mkoa wa Magomeni umesema kuwa kuna baadhi ya wananchi wanahujumu miundombinu ya shirika hilo pamoja kuunganisha umeme bila malipo ya ankara.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika operesheni ya ukaguzi wa mita za umeme katika Mkoa huo Mhandisi wa Udhibiti wa Mkoa wa Tanesco Magomeni Lukaluka Kapinga amesema kuna baadhi ya  wananchi wanaunganisha umeme nje ya utaratibu pamoja na kuchepusha umeme katika mfumo wa mita.

Mhandisi Lukaluka amesema baadhi ya wananchi wananunua mita za umeme za wizi ambapo katika operesheni hiyo wamebaini kuwepo kwa mita katika nyumba ya Msikiti wa Kichangani Magomeni mapipa kuwa na Mita inayosoma Kimara-Mbezi.

Pia amesema kuwa katika operesheni hiyo wamewataka wananchi kufuata tararibu za uombaji wa umeme na kutotumia watu ambao mwisho wa siku wanawaingiza wananchi hatari ya kulipa faini pindi wanapokutwa wamejiunganishia umeme nje ya utaratibu.

Kwa upande wake Ofisa Usalama wa Mkoa wa Tanesco Magomeni  Jane Komba amesema katika operesheni hiyo hawatamuacha mtu salama ambaye ameungansha umeme nje ya utaratibu.Amesema kuwa vishoka wanaingiza wananchi katika matatizo kwa kukosa taarifa sahihi za maandishi kutoka kwa vishoka hao.
 Mita ya  Umeme iliyounganishwa  bila kupita katika mfumo wa kuilipa ankara katika moja ya nyuma Eneo la Tandale jijini Dar es Salaam.
Mita ya Umeme ikininginia katika Mti ambapo ni kinyume na utaratibu wa Tanesco hali ambayo ililazimu kuondoa na kuweka utaratibu mpya wa kuomba kuweka mita hiyo.
 Mhandisi wa Taneso wa Mkoa wa Magomeni Lukaluka Kapinga akikata umeme kwenye nyumba ambayo mmliki wa nyumba kachepusha umeme kwa kulipa kiwango kidogo katika eneo Kigogo Mpera jijini Dar es Salaam. 
 Mhandisi wa Taneso wa Mkoa wa Magomeni Lukaluka Kapinga akikata umeme kwenye nyumba kwa ambapo Mita yake inasoma Kimara wakati Mita Iko Magomeni mapipa ikiwa ni Mali ya Msikiti wa Kichangani jijini Dar es Salaam.
Afisa Usalama wa Tanesco Mkoa wa Magomeni Jane Komba akizungumza na waandishi habari kuhusiana wananchi kuunganisha umeme bila kufuata utaratibu wa Tanesco jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...