Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
RAIS wa Marekani Donald Trump kupitia ukurasa wake wa Twitter ameweka picha ya mbwa ambaye alisaidia vikosi vya ulinzi katika zoezi la kumkamata na kumuua kiongozi wa kikundi cha ugaidi cha ISIS Abu Bakr al -Baghdadi.

Katika picha hiyo Rais Trump ameeleza kuwa, mbwa huyo alishirikiana na timu ya vikosi maalumu ya ulinzi katika zoezi la kumkamata na kumuua kiongozi wa kundi la kigaidi la ISIS  ambapo katika tukio hilo Baghdadi alijilipua akiwa na watoto watatu ndani ya handaki na mbwa huyo kujeruhiwa.

Taarifa zimeeleza kuwa jina la mbwa huyo bado halijafahamika na bado anapatiwa matibabu ambapo hali yake imeendelea kuimarika vizuri baada ya kutolewa katika chumba cha upasuaji na baadaye atarejea katika majukumu kawaida na taarifa zake zitaendelea zinatunzwa.

viongozi mbalimbali wa jeshi akiwemo Rais wa shirikisho la mbwa wa kivita nchini Marekani Ron Aiello wamempongeza mbwa huyo kwa kupambana katika shambulio hilo huku wengi wakieleza kuwa aina ya mbwa anayetakiwa kuongoza doria ni wa aina hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...