Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL Corporation, Waziri Kindamba (kulia) akisaini hati ya makubaliano na Mtendaji Mkuu wa Mfumo wa Mawasiliano ya Taifa la Burundi (Burundi Backbone Systems-BBS), Elie Ntihagowumwe (kushoto) ya BBS kupewa huduma za mawasiliano na TTCL Corporation. Nyuma yao ni wanasheria wa pande zote mbili wakishuhudia tukio hilo. 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania -TTCL Corporation, Waziri Kindamba (wa pili kulia) pamoja na Mtendaji Mkuu wa Mfumo wa Mawasiliano ya Taifa la Burundi (Burundi Backbone Systems-BBS), Elie Ntihagowumwe wakibadilishana nakala za makubaliano ya kibiashara mara baada ya kusainiwa leo. Katika makubaliano hayo TTCL Corporation itatoa huduma za mawasiano kwa BBS kwa muda wa miaka 10. 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania -TTCL Corporation, Waziri Kindamba (kulia) akizungumza katika tukio hilo. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Dk. Jim Yonaz akishuhudia tukio hilo na Mtendaji Mkuu wa Mfumo wa Mawasiliano ya Taifa la Burundi (Burundi Backbone Systems-BBS), Elie Ntihagowumwe (kushoto). 
Mtendaji Mkuu wa Mfumo wa Mawasiliano ya Taifa la Burundi (Burundi Backbone Systems-BBS), Elie Ntihagowumwe (kushoto) akimpa zawadi Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania -TTCL Corporation, Waziri Kindamba kama ishara ya shukrani mara baada ya hafla hiyo. 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania -TTCL Corporation, Waziri Kindamba (kulia) akimpa zawadi Mtendaji Mkuu wa Mfumo wa Mawasiliano ya Taifa la Burundi (Burundi Backbone Systems-BBS), Elie Ntihagowumwe kama shukrani kwa uhusiano kibiashara kwa pande mbili. 


SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL-Corporation) limeingia makubaliano ya kibiashara na Taasisi ya Serikali ya Nchini Burundi inayosimamia Mawasiliano ya Mkongo wa Taifa wa nchi hiyo, Burundi Backbone System (BBS) ili TTCL kuwezesha mawasiliano katika taifa hilo.

Makubaliano hayo yamefikiwa leo jijini Dar es Salaam na yatadumu kwa takribani miaka 10 huku yakihusisha, TTCL Corporation kutoa huduma za data na intaneti zijulikanazo kwa kitaalamukama IP TRANSIT, BACKHAULING pamoja na huduma ya IPLC.

Akizungumza katika hafla ya kusaini makubaliano hayo, Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Corporation, Bw. Waziri Kindamba alisema hatua hiyo ni ya mafanikio kwani TTCL litakuwa ni Shirika pekee linalotoa huduma ya Mawasiliano ya Mkongo Nchini Burundi kupitia vituo vyake vya mpakani katika miji ya Kabanga na Manyovu, na kuiunganisha nchi ya Burundi na Dunia kupitia Mikongo mikubwa ya baharini SEACOM na EASY.

Waziri Kindamba alibainisha kuwa makubaliano hayo ya kibiashara yenye thamani ya shilingi Bilioni 13.8 yatahusisha TTCL Corporation kutoa huduma za Utunzaji wa kumbukumbu mbadala kupitia kituo cha kimataifa cha kutunzia kumbukumbu 'National Internet Data center' cha jijini Dar es Salasam, pamoja na kubadilishana wataalamu kwa kujengeana uwezo kitaalamu nyanja mbalimbali za Mawasiliano.

"Mabadilishano ya wateja hasa kwa wateja wakubwa wenye matawi ya biashara au ofisi katika nchi zote mbili (Burundi na Tanzania) kwa mfano CRDB BANK, pia kupeana ushauri wa kitaalamu kuhusu watoa huduma na watengenezaji wakubwa wa vifaa vya Mawasiliano vinavyotumika kuhudumia Mawasiliano ya Mkongo (Fiber and Terminal Equipment Suppliers Advisory)."

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Mfumo wa Mawasiliano ya Taifa la Burundi (Burundi Backbone Systems-BBS), Elie Ntihagowumwe aliishukuru Tanzania kupitia TTCL kwa kuendelea kushirikiana kibiashara na masuala mengine mengi ambayo Tanzania imekuwa ikiisaidia nchi ya Burundi.

Alisema mbali na makubaliano hayo ya kibiashara Burundi itanufaika kwa mengi haswa kujifunza kutokana na hatua ambazo taifa la Tanzania limepiga kwa sasa ukilinganisha na taifa la Burundi.

"...Kimsingi tunashukuru kwa uhusiano huu wa kibiashara tulioingia leo. Hata hivyo taifa letu lina mengi ya kujifunza na kunufaika kutoka Tanzania hasa kwa hatua Tanzania imepiga kwa sasa," alisema Mtendaji Mkuu wa BBS, Ntihagowumwe. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...