Wakati msimu wa kumi wa mbio za Rock City Marathon ukihitimishwa kwa kushirikisha mamia ya wanariadha kutoka ndani ya nje ya nchi, Serikali imesema ipo haja ya kufanya tathmini ili kupima mchango wa mbio za aina hiyo katika kuinua sekta ya utalii hapa nchini ili iweze kuwekeza nguvu zaidi katika kuziboresha.

Akizungumza wakati wa kilele cha mbio hizo zilizofanyika kwenye viunga vya jengo la Biashara la Rock City Mall ambapo ilishuhudiwa wakimbiaji kutoka nchini Kenya wakiendelea kutamba, Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. HamisI Kingwalla alisema wingi wa wawashiriki kutoka ndani na nje ya nchini ni kiashilio tosha kuwa mbio hizo zikitumika vizuri kutangaza utalii zitachochea ukuaji wa sekta hiyo muhimu kiuchumi.

“Nimeshuhudia mamia ya washiriki kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini wamekuja kushiriki mbio hizi,tayari hiyo ni sehemu ya utalii wa ndani. Zaidi imeshuhudiwa ushiriki wa wenzetu kutoka nje ya nchini ikiwemo Kenya,Rwanda na wengine nje ya bara la Africa nao wamekuja.’’

“Ili kupata mchango hasa wa mbio kama hizi kwenye sekta ya Utalii na ukuaji wa uchumi naagiza ufanyike utafiti wa kisayansi ili Serikali tujue namna ya kuziunga mkono ziendelee kufanya vizuri zaidi,’’ aliagiza Dr Kigwangalla ambae pia alishiriki kukimbia mbio za Km 21.

Tangu kuanzishwa kwa mbio miaka 10 iliyopita zimekuwa zikivutia zaidi washiriki kutoka mataifa ya Kenya na Rwanda ambapo ilishuhudiwa Mwanariadha Kutoka Kenya Ibrahimu Too akiibuka mshindi wa mbio za km 42 upande wa wanaume baada ya kutumia muda wa 2:18:34 akifuatiwa na Wakenya wenzake Willium Koskei na John Muthui waliotumia muda wa 2:19:06 na 2:21:30 kila mmoja.Mtanzania pekee kwenye kumi bora wanaume alikuwa Hamis Athumani aliefanikiwa kushika nafasi ya nne huku akitumia muda wa 2:21:36

Kwa upande wa wanawake katika mbio hizo za km 42 ilishuhudiwa mwanariadha Elilither Tamui kutoka Kenya akiibuka mshindi baada ya kutumia muda wa 2:42:50 akifutiwa na wakenya wenzake Joan Rotich (2:46:07) na Lydia Wafula (2:48:57) ambapo Watanzania Fabiola John na Zainabu Hamis walifanikiwa kushika nafasi ya 6 na nafasi ya 10.

Katika mbio za Km 21 mshindi wa kwanza upande wa wanaume ni Bernard Musau kutoka Kenya alietumia muda wa 01:11:26 akifuatiwa na Ochieng Julius kutoka Uganda alitumia muda wa 01:11:36 huku mshindi wa tatu akiwa ni Alex Nizemana kutoka Rwanda alitumia muda wa01:12: 21

Kwa upande wanawake katika mbio hizo za km 21 mshindi wa kwanza hadi wa nne wote ni kutoka Kenya ambao ni Ester Kakuri alietumia muda wa 1:21:44 , Vane Nyaboke (1:22:13), Ronah Nyabochoa (1:23:10) na Martha Njoroge(1:23:17) huku mshindi wa tano ni Grace Jackson kutoka Tanzania alietumia muda wa 1:24:23

Akizungumzia matokeo hayo Mshauri wa Masuala ya Ufundi wa Mbio hizo Bw John Bayo pamoja na kuwapongeza wanariadha kutoka Kenya kwa kufanya vizuri alisema kuwa Tanzania haikupata ushiriki wa wanariadha wakubwa kutokana na wengi wao kushiriki kwenye mbio za kimataifa na hivyo kutoa mwanya kwa wanariadha hususani wa Kenya kuweza kutamba kwenye mbio hizo.

Mbio hizo zilipambwa kupambwa na burudani mbalimbali zikiwemo ngoma za asili na maonesho ya waadau mbalimbali wa utalii pamoja na wadhamini wa mbio hizo ikiwemo Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) sambamba na wadhamini wa mbio hizo ambao ni pamoja na kampuni za TIPER na Pepsi.

Wadhamini wengine ni pamoja na, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), CF Hospital, Metro FM, Mwanza Water, Pigeon Hotel, The Cask and Grill, SDN na Kampuni ya Ulinzi ya Garda World.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. HamisI Kingwalla (katikati) akimpatia zawadi ya fedha taslimu kiasi cha Sh milioni 4/- mshindi wa mbio za Rock City Marathon Km 42 kwa upande wa wanawake Bi Elilither Tamui kutoka Kenya alieibuka mshindi baada ya kutumia muda wa 2:42:50. Wengine ni pamoja na Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Kuhifadhi Mafuta ya TIPER, Bw Emmanuel Kondi (kulia) ambao ni moja ya wadhamini wakubwa wa mbio hizo zilizofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viunga vya Jengo la Biashara la Rock City Mall jijini Mwanza.
Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Kuhifadhi Mafuta ya TIPER, Bw Emmanuel Kondi (katikati) akimpatia zawadi ya fedha taslimu mmoja wa washindi wa mbio za Rock City Marathon Km 21.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. HamisI Kingwalla (wa pili kulia) akishiriki mbio za km 21 za RockCity Marathon sambamba na mamia ya washiriki wengine wa mbio hizo.
Baadhi ya matukio yaliyopamba mbio za Rock City Marathon msimu wa 10 jijini Mwanza.














Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...