Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
KIKOSI cha   Yanga kesho kinatarajia kushuka dimbani kucheza mchezo wake wa pili kirafiki dhidi ya Pan African utakaochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Yanga walicheza mchezo wa kwanza dhidi ya Friends Rangers kwenyw Uwanja wa Polisi Kurasini na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 4-3.

Mkuu wa Kitengo cha Habari Yanga, Hassan Bumbuli amesema mchezo huo utakuwa ni muendelezo wa kujiweka sawa kwa ajili ya michezo ya Ligi kuu pamoja Mchezo wa hatua ya mtoano wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Pyramids.

Bumbuli amesema, timu itakuwa chini ya Kocha Noel Mwandila ambaye atasimamia timu mpaka hapo Kocha Mkuu Mwinyi Zahera atakaporejea kutoka kwenye majukumu ya timu yake ya Taifa.

Amesema, wachezaji waliokuwa majeruhi wameanza mazoezi isipokuwa Mohamed Issa 'Banka' ambaye bado anauguza majeruhi yake.

" Wachezaji wote waliokuwa majeruhi wameanza mazoezi isipokuwa Banka, Pauk Godfrey tayari amejumuika na wenzake na hata  Yondani  aliyeshindwa kwenda kwenye majukumu ya timu ya Taifa ameanza mazoezi jana,"amesema Bumbuli.

Yanga baada ya kumaliza mchezo wake wa Kesho, watajiandaa na safari ya kwenda Mwanza kuiwinda na michezo miwili ya Ligi Kuu dhidi ya Mbao na Alliance na kisha kumalizia na mchezo wao dhidi ya Pyramids.

Mchezo wa Yanga dhidi ya Pan Africa utachezwa majira ya saa 10 alasiri.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...