Sehemu ya Ujumbe wa  Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora wakiwamo Makamisha  wakati walipomtembelea ( Courtesy Call) Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

 Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Kilangi (AG) akimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jaji Mstaafu Mhe. Methew Mwaimu  wakati  yeye na Makamisha wanaounda Tume hiyo walipomtembelea Mwanasheria  Mkuu wa Serikali na kufanya naye mazungumzo.
Sehemu ya Ujumbe wa  Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora wakiwamo Makamisha  wakati walipomtembelea ( Courtesy Call) Mwanasheria Mkuu wa Serikali.


DODOMA , Nov 13,2019 

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Kilangi ( AG)leo ( jumatano) amekutana na kisha kuwa na mazungumzo na Ujumbe wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora. 

Mazungumzo baina ya AG na Tume hiyo ambayo iliongozwa na Mwenyekiti wake Jaji Mstaafu Mhe. Methew Mwaimu yamefanyika katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali iliyopo katika Mji wa Kiserikali Mtumba Jijini Dodoma. 

Mwenyekiti wa Tume hiyo Mhe. Jaji Mstaafu Methew Mwaimu alimueleza Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kwamba, Madhumuni ya ziara hiyo pamoja na masuala mengine, yalikuwa ni kujitambulisha kwake lakini pia kujadiliana na kubadilishana mawazo ya namna Ofisi hizo mbili zinaweza kushirikiana kwa karibu katika utekelezaji wa majukumu yao. 

Kwa upande wake Profesa Kilangi, aliishukuru Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora wa kuona umuhimu wa kumtembelea na kubadilishana naye mawazo ikiwa ni muda mfupi tangu kuteuliwa kwao na kuapishwa kwao. 

AG ameihahidi tume hiyo ushirikiano madhubuti kutoka katika Ofisi yake. 
Mazungumzo hayo pia yalihudhuriwa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Evaristo Longopa na Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu na Huduma za Kisheria, Dkt. Gift Kweka. 

Itakumbukwa kwamba Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mhe. Jaji Mstaafu Methew Mwaimu na Makamisha wake waliteuliwa Mwezi Septemba mwaka huu na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...