Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, CGP – Phaustine Kasike akipokea msaada wa
baiskeri ya walevu pamoja na vitu mbalimbali vilivyotolewa na Asasi ya
Kidini ya New Life In Christ leo Novemba 15, 2019 kwa ajili ya wafungwa.
Hafla ya upokeaji wa misaada hiyo imefanyika katika gereza Kuu Karanga
Moshi.
Muonekano
wa baadhi ya misaada ya Kibinadamu iliyotolewa Asasi ya Kidini ya New
Life In Christ iliyokabidhiwa kwa Jeshi la Magereza leo Novemba 15, 2019
katika viwanja vya Gereza Kuu Karanga Moshi. Misaada imekabidhiwa leo
kwa ujumla wake ina thamani ya zaidi ya milioni 183.
Mhandisi
ujenzi wa Jeshi la Magereza, SP. Julius Sukambi akitoa maelezo ya
kitaalam kwa Kamishna Jenerali wa Magerezanchini, CGP – Phaustine Kasike
alipotembelea katika eneo hilo la ujenzi wa Kiwanda Kipya cha bidhaa za
ngozi kinachojengwa nje ya eneo la Gereza Kuu Karanga, Moshi
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, CGP – Phaustine Kasike akisalimiana na
Meneja Miradi wa Asasi ya Kidini ya New Life In Christ Mkoani
Kilimanjaro, Bw. Charles Shang’a alipowasili katika viwanja vya Gereza
Kuu Karanga Moshi kwa ajili ya hafla fupi ya kupokea Misaada ya
Kibinadamu iliyotolewa na Asasi hiyo kwa ajili ya wafungwa leo Novemba
15, 2019.
Meza
kuu wakiongozwa na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP –
Phaustine Kasike (wa pili toka kushoto) wakiimba wimbo wa Taifa la
Tanzania ikiashiria ufunguzi wa hafla fupi ya kupokea misaada ya
Kibinadamu kwa ajili ya wafungwa iliyotolewa na Asasi ya Kidini ya New
Life In Christ. Tukio hilo limefanyika leo Novemba 15, 2019 katika
viwanja vya Gereza Kuu Karanga Moshi.
Kaimu
Mkurugenzi wa Asasi ya Dorcas Aid International Tanzania Bw. Joseph
Kumwembe akitoa maelezo mafupi kabla ya kukabidhi msaada wa Kibinadamu
kwa ajili ya Wafungwa nchini. Dorcas Aid International Tanzania
hushirikiana na Asasi ya Kidini ya New Life In Christ katika kutoa
misaada ya namna hiyo.
Kamishna
Jenerali wa Magerezanchini, CGP – Phaustine Kasike akitoa hotuba kwa
wageni mbalimbali (hawapo pichani) waliohudhuria hafla fupi ya kupokea
msaada wa Kibinadamu kwa ajili ya wafungwa kutoka kwa Asasi ya Kidini ya
New Life In Christ leo Novemba 15, 2019 katika viwanja vya Gereza Kuu
Karanga Moshi.
(Picha zote na Jeshi la Magereza).
…………………..
Na ASP Lucas Mboje, Moshi
ASASI
ya Kidini ya New Life In Christ imekabidhi kwa Jeshi la Magereza
misaada ya vitu mbalimbali yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni
183 ambayo itawanufaisha wafungwa na Mahabusu waliopo magerezani katika
Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Tanga.
Akizungumza
kabla ya kukabidhi misaada hiyo ya wahalifu waliopo magerezani, Kaimu
Mkurugenzi wa Asasi ya Dorcas Aid International Tanzania, Bw. Joseph
Kumwembe amesema vifaa vilivyokabidhiwa ni magodoro, sabuni, nguo za
watoto, mabranketi, vipeperushi, vifaa vya usafi na vitabu vya kiroho.
Kwa
upande wake, Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike
ameishukru Asasi hiyo isiyo ya Kiserikali kwa kuendelea kuunga mkono
juhudi za Serikali katika kutekeleza kwa ukamilifu utoaji wa misaada ya
kibinadamu pamoja na baadhi ya huduma muhimu kwa wafungwa ikiwemo
mafunzo ya Kijasiriamali kwa wafungwa hivyo kulisaidia Jeshi la Magereza
katika suala zima la urekebishaji wa wafungwa.
“Niwashukru
sana Asasi hii kwa moyo wao wa upendo na kujitolea na niwapongeze sana
kwa kutambua kwamba wahalifu waliopo magerezani ni Binadamu kama walivyo
Binadamu wengine na wanahitaji misaada ya ki-binadamu kama hii,”
Amesema Jenerali Kasike.
Aidha,
Jenerali Kasike ametoa wito kwa Asasi nyingine zisizo za Kiserikali
kuiga mfano uliooneshwa na New Life in Christ na Dorcas Aid
International Tanzania ili ziweze kushirikiana na Jeshi la Magereza kwa
manufaa ya Taifa.
Katika
hatua nyingine, Kamishna Jenerali Kasike amewataka Wakuu wote wa
Magereza yaliyonufaika na misaada hiyo kuhakisha kuwa misaada
inawanufaisha walengwa kwa maeneo yaliyokusudiwa samabamba na kusimamia
vyema vifaa hivyo.
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike mara baada ya kupokea
misaada hiyo ametembelea eneo la mradi mkubwa wa uwekezaji wa Kiwanda
kipya cha bidhaa za ngozi ambacho ni cha ubia kati ya Jeshi la Magereza
pamoja na Mfuko wa hifadhi ya jamii wa PSSSF. Kiwanda hicho kinajengwa
katika eneo lililopo nje ya Gereza Kuu Karanga, Moshi ambapo
amewasisitiza wakandarasi wa ujenzi huo kufanya kazi usiku na mchana ili
kukamilisha mradi huo kwa wakati.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...