Mkurugenzi Mtendaji  wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Godfrey Sembeye akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutambulisha mkutano wa wafanyabiashara wa nchi za Juimuiya ya Afrika Mashariki.
Mkurugenzi Mtendaji  wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Godfrey Sembeye katikati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutambulisha mkutano wa wafanyabiashara wa nchi za Juimuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika Novemba 28,29, mwaka huu jijini Arusha. Kulia ni Mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa Afrika mashariki Emma Oriyo na kushoto ni Mwakilishi wa EABC, Raphael Maganga.
 Baadhi ya waandishi wa Habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji  wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Godfrey Sembeye jijini Dar es Salaam leo.

Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii
BARAZA la Biashara la Afrika Mashariki (EABC) linatarajia kusheherekea miaka 20 tangu kuanzishwa kwake pamoja na kufanya mkutano wa kujitadhimini.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji  wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Godfrey Sembeye, amesema kuwa mkutano huo unatarajiwa kufanyika Novemba 28-29, 2019 jijini Arusha kwa kuwakutanisha wafanyabiashara wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Amesema kuwa mada kuu katika mkutano huo itakuwa ni kuangalia masuala ya kodi kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, kuangalia minyonyoro ya thamani, kuangalia viwango vya bidhaa, gharama za usafirishaji, muda wa usafirishaji pamoja na mawasiliano katika biashara.

Aidha Sembeye amesema kuwa wanatarajia marais wa nchi hizi za Afrika Mashariki kuhudhuria ingawa kuna baadhi ya viongozi hawajathibitisha kama watahudhuria katika mkutano huo.

"Tunategemea marais wote wa Afrika Mashariki watahudhuria kwenye Mkutano wa Biashara na uwekezaji kabla hawajajumuika kwenye mkutano wa Viongozi ambao unatarajiwa kufanyika Novemba 30, 2019", amesema Sembeye.

Kwa Upande wake Mwakilishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Raphael Maganga amesema zaidi ya wafanyabishara zaidi mia tano wanatarajia kuhudhulia mkutano huo. 

Amesema ni nafasi nzuri kwa watanzania kuangalia fursa za kuanza kuwauzia majirani bidhaa mbalimbali kwa hiyo kongamano hilo walitumie vizuri.

Washiriki ni wafanyabiashara wa Nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo ni Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania, Uganda na Sudani Kusini. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...