Mkaguzi na Mdbiti Mkuu wa Hesabu za Serikali aliyemaliza muda wake Profesa Mussa Assad akizungumza mara baada ya makabidhiano ya nyaraka na CAG mpya Charles Kichere katika hafla iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mpya, Bw. Charles Kichere amesema kuwa ataendelea kutekeleza majukumu ambayo yameachwa na CAG aliyemaliza muda wake Prof.Mussa Assad kwani Ofisi hiyo ni muhimu kwa maendeleo ya watanzania.

Akizungumza katika makabidhiano Kichere alisema kuwa Ofisi ya CAG ni nguzo muhimu kwa watanzani kwani ndiyo ofisi inayolinda na kuangalia matumizi sahihi ya kodi yao wanayolipa kila siku.

“Tutaendelea kuifanyakazi ambayo imefanywa na Prof.Assad na timu yake, nitahakikisha kushirikiana na wafanyakazi wa Ofisi hii kuifanya kazi hii ya kulinda mapato ya kodi ya watanzania”, Alisema Kichere.

Kichere alisema kuwa katika kutekeleza majukumu hayo mapya atahakikisha kuwa atalinda Kodi ya watanzania wakulima, wafugaji, wavuvi, wafanyabiashara na wafanyakazi ili fedha inayopataikana kwenye kodi iweze kuwanufaisha wote.

Aliwahakikishia watanzania kuwa hakuna kodi inayotolewa na watanzania ambayo itapotea kwa hiyo ataangalia na kuilinda  kwaajili ya kuwaletea maendeleo.

“Nataka kufanya kazi kulinda maslahi ya watanzania nimefanyakazi Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA najua ugumu wa kukusanya kodi na kupata mapato, kwa hiyo nitahakikisha kuwa nailinda kodi ya wananchi kwa wivu mkubwa sana”, Alisisitiza Kichere.

Kwa upande wake CAG aliyemaliza muda wake Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) aliyemaliza muda wake Profesa Mussa Assad amesema kuwa anakwenda kufanya kilimo kutokana na uwekezaji alioufanya katika siku hivi karibuni baada ya kustaafu nafasi hiyo, akinadi kwamba  watu mjini wakinihitaji nitakuja .

Profesa Assad ameyasema hayo wakati wa makabidhiano na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mpya Charles Kichere katika hafla iliyofanyika kwenye Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT),leo  jijini Dar es Salaam.

Profesa amesema kuwa katika kufanya kazi amewashukuru wafanyakazi wa ofisi hiyo kwa ushirikiano waliompa katika kipindi chote cha utumishi na kumtaka CAG mpya afanye ushirikiano nao kwani watu hao wamejengwa kwa muda mrefu na sifa zote .

Assad amesema kuwa katika kufanya kazi tumejenga mahusiano na wadau mbalimbali wa nje ambao ndio watu wa kujengeana uwezo na sio kwa ndani

“Changamoto ni nyingi tumepitia lakini siwezi kutia ukakasi katika hili na watu  niliowakosea, naomba wanisamehe kwani sisi ni binadamu”amesema Profesa Assad

Kwa upande wa CAG Charles Kichere mpya amesema kuwa kazi kubwa ni kulinda kihenge anajua kazi ngumu ya ukusanyaji wa mapato.

Kichere amesema ataifanya kazi hiyo kwa weledi na uadilifu kwa kushirikiana na timu yake ya ofisi ya Taifa ya mkaguzi ikiwa na kuangalia mapato ya nchi yanatumikaje kwa kuangalia ripoti sambamba na kujenga timu imara na sio watu walisambaratika.
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali aliyemaliza muda wake Profesa Mussa Assad akimkabidhi nyaraka za ofisi CAG mpya Charles Kichere katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. 
Mkaguzi na Mdbiti Mkuu wa Hesabu za Serikali aliyemaliza muda wake Profesa Mussa Assad akizungumza mara baada ya makabidhiano ya nyaraka na CAG mpya Charles Kichere katika hafla iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mpya Charles Kichere akizungumza mara baada ya kukabidhiwa na aliyekuwa CAG Profesa Mussa Assad katika hafla iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG) Mpya Charles Kichere akiwa na maua mara baada ya kupokewa wakati akiwasili katika ofisi ya Taifa ya Ukaguzi kwa ajili ya makabidhiano ya Ofisi ya aliyekuwa CAG Profesa Assad jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...