Na Woinde Shizza michuzi Tv,Arusha

Mkuu wa Arusha ,Mrisho Gambo amewataka wakandarasi kutumia mabenki kuchukua mikopo ili kuwawezesha kukamilisha miradi yao kwa wakati na kuacha kutegemea malipo ya awali ya mradi husika ambazo zimekuwa zikichelewa na kufanya miradi kutokamilika kwa wakati.

Ameyasema hayo leo wakati akizungumza katika kongamano lililowashirikisha wakandarasi ,wazabuni  na wadau wa benki ya CRDB lengo likiwa ni kuwapatia elimu juu ya matumizi sahihi ya fedha za mikopo wanazozichukua kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali.

Amesema kuwa,wakandarasi ni sekta muhimu Sana katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini hivyo wanapaswa kuboresha utendaji  kazi wao kwa kuchukua mikopo toka taasisi za fedha na mabenki.

Hata hivyo Gambo alipongeza benki ya CRDB kwa kuanzisha huduma ya 'niwezeshe "mikopo ambayo imekuwa ikitolewa kwa wafanyabiashara wadogo hasa wamachinga.

Ameongeza kuwa,changamoto kubwa inayowakabili wakandarasi wengi ni ukosefu wa mitaji kwa ajili ya kuendesha miradi mbalimbali ambapo changamoto hiyo huchangia kutomalizika kwa miradi kwa wakati.

Ameongeza kuwa,benki hiyo imekuwa benki ya kimkakati inayofuata misingi ya serikali katika kupambana katika kukuza uchumi na kuchangia kuunga mkono miradi mikubwa ya kimkakati inayoanzishwa na serikali.

Awali Mkurugenzi wa wateja wa Kati na wadogo ,Boma Rabala amesema kuwa,kongamano hili ni fursa pekee ya kuwakutanisha wazabuni na wakandarasi ili kuwajengea uwezo namna ya kutumia fursa za kibenki zinazoanzishwa na benki hiyo.

Amesema kuwa,hivi karibuni benki hiyo imeanzisha huduma ya mikopo kwa wafanyabiashara wadogo 'machinga'inayofahamika kama jiwezeshe kwa ajili ya kuwapatia mikopo isiyo na masharti yoyote inayoanzia shs 10,000  hadi 500,000 lengo ni kuhakikisha wafanyabiashara hao wanakuwa na mikopo ya kutosha.

Ameongeza kuwa,benki hiyo ambayo ni ya kizalendo kwa kuelewa changamoto imeamua kuja  na huduma ambayo inaendana na mazingira ya kitanzania ili kuwawezesha wazabuni na wakandarasi kuweza kupata mkopo wa haraka ambao hauna masharti ambayo inachukua muda mrefu.

Naye mmoja wa Wakandarasi Felix Nnko ambaye ni Mkurugenzi wa  kampuni ya Felix constructors T Ltd , amesema kuwa,swala zima la uwezeshwaji wa mikopo hiyo litawasaidia kwa kiasi kikubwa sana wakandarasi hao kumaliza miradi yao kwa wakati kwani changamoto kubwa ilikuwa ni mitaji kwa ajili ya kuendeleza miradi yao.

Amesema kuwa,kinachotakiwa kikubwa ni uaminifu wa wakandarasi katika kujua fedha wanayopewa inahitaji kufanyiwa  kazi na kurudishwa kwa wakati.

Naye mkandarasi mwingine kutoka  kampuni ya Raz Builders T Ltd,Zuberi Abdallah amesema kuwa,wanashukuru sana benki hiyo kuja na ubunifu wa kuwapatia mikopo kwani changamoto kubwa ilikuwa katika upatikanaji wa mikopo,ila kwa sasa hivi wana imani wataboresha shughuli zao.

 Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akifungua  kongamano lililowashirikisha wakandarasi ,wazabuni  na wadau wa benki ya CRDB lililofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Mounti Meru.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...