Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo,akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji, Wajibu, Bw.Ludovick Utuoh,kabla ya kufunga Mkutano wa Mijadala ya wiki ya AZAKI iliyohitimishwa leo jijini Dodoma baada ya kuanza Novemba 4 hadi 8 mwaka huu.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo,akizungumza,na wadau kutoka Asasi za Kiraia wakati akifunga Mkutano wa Mijadala ya wiki ya AZAKI iliyohitimishwa leo jijini Dodoma baada ya kuanza Novemba 4 hadi 8 mwaka huu.
Rais wa Foundation for Civil Society, (FCS), Dkt Stigmata Tenga,akitoa taarifa kuhusu jinsi Wiki ya AZAKI ilivyokuwa katika maonesho hayo ambayo yalianza Novemba 4 hadi leo Novemba 8 ambapo yamefungwa na Waziri wa TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo
Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi CCM Mhe.Humphrey Polepole,Akizungumza wakati wa kufunga mkutano wa majadiliano ya Wiki ya AZAKI ambayo yalianza jijini Dodoma Novemba 4 hadi leo Novemba 8.
Mkurugenzi Mtendaji, Wajibu, Bw.Ludovick Utuoh, Akizungumza wakati wa kufunga Maonesho ya wiki ya AZAKI ambayo yalianza jijini Dodoma Novemba 4 hadi leo ambapo yamefungwa na Waziri wa TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo,akisisitiza jambo kwa washiriki kutoka Taasisi mbalimbali za Asasi za Kiraia wakati akifunga Mkutano wa Mijadala ya wiki ya AZAKI iliyohitimishwa leo jijini Dodoma baada ya kuanza Novemba 4 hadi 8 mwaka huu.
Sehemu ya washiriki wa Taasisi za Asasi za Kiraia wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo (hayupo pichani) wakati akifunga maonesho ya wiki ya AZAKI yaliyomalizika leo jijini Dodoma.
Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya uwezeshaji Asasi za kiraia(FCS), Francis Kiwanga,akizungumza na washiriki kutoka Taasisi mbalimbali za Asasi za Kiraia wakati wa kufunga mkutano wa majadiliano ya wiki ya AZAKI.
Mratibu ,Wiki ya AZAKI 2019 Justice Rutenge,akitoa taarifa ya hitimisho ya Wiki ya AZAKI ambapo maonesho hayo yamefikia mwisho na kufungwa na Waziri wa TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo yalianza jijini Dodoma Novemba 4 hadi leo Novemba 8,2019.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo,akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Asasi za Kiraia (AZAKI) ambapo maonesho hayo yameitimishwa leo jijini Dodoma.


JAFO AZIAGIZA HALMASHAURI NCHINI KUHARAKISHA VIBALI VYA AZAKI, "HAWA NI WADAU WA MAENDELEO"

Charles James, Michuzi TV

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuhakikisha anasimamia zoezi la utoaji wa vibali vya usajili wa Asasi za Kiraia (Azaki) bila kuchelewesha.

Mhe Jafo amesema agizo hilo linakwenda pia kwa Mikoa na Halmashauri zote nchini kuharakisha kutoa vibali kwa Azaki zinazotuma maombi ya usajili ili kwa kuwa Azaki hizo zimekua mstari wa mbele katika kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali kuwaletea wananchi maendeleo.

Agizo hilo limetolewa leo jijini Dodoma wakati Mhe Jafo alipokua akifunga maadhimisho ya wiki ya Azaki yaliyodumu jijini hapa kwa juma zima na kuhudhuriwa na Azaki 500 na Taasisi 100.

Waziri Jafo amezitaka Asasi za kiraia nchini kuwa mabalozi wazuri katika kusemea mambo mema yanayofanywa na Serikali chini ya Rais Dk John Magufuli na kuzitama kusimamia malengo waliyojiwekea.

Mhe Jafo amesema kumekuepo na malalamiko kwenye Ofisi yake kuhusiana na kucheleweshwa kwa usajili wa Asasi hizo pindi wanavyoomba maombi ya usajili na kuwaahidi kuwa hata ikiwabidi kuomba kwenye Ofisi yake yupo tayari kusaini yeye mwenyewe.

Amesema maendeleo mengi yanayofanywa na Serikali hivi sasa kwenye sekta mbalimbali za Afya, Elimu, Miundombinu na Utawala bora yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na ukosoaji uliokua ukitolewa na Azaki hivyo ni vema wakapewa ushirikiano kwani wamekua ni wadau wa maendeleo nchini.

"Nakuagiza Katibu Mkuu wa Ofisi yangu hakikisha vibali vinatolewa bila vikwazo kwa Asasi hizi, ili mradi ina manufaa kwa Taifa na jamii kwa ujumla,na pia iwe na Sera zinazoeleweka katika kuchagiza maendeleo," amesema Jafo.

Amesema maendeleo mengi yanayofanywa na Serikali ya awamu ya tano,yametokana na mchango wa AZAKI wa kuibua changamoto zilizopo katika sekta mbalimbali hapa nchini,hivyo AZAKI zinastahili kupongezwa na kuskilizwa.

"Naomba niwapongeze sana AZAKI mmekuwa mkiibua matatizo yaliyopo sehemu tofauti, kwa mfano Hakielimu na tangazo lao la shule mbovu, yamesaidia serikali imeona na kuwekeza fedha nyingi katika sekta ya elimu kwa ajili ya kuziboresha na kufanya ujenzi.

"Katika sekta ya afya pia,barabara note mmekuwa mkipasemea na hivi sasa serikali inayafanyia kazi yote,na matokeo yanaonekana katika sekta hizo zilivyoimarika," Amesema Waziri Jafo.

Pamoja na hayo pia ameziagiza Asasi hizo za kiraia kuhakikisha wanasaidiana katika kuwezeshana na kurekebishana na sio kusemeana vibaya ili asasi nyingine zife jambo ambalo halikubaliki.

Amezitaka AZAKI hizo kuendelea kusaidia kulinda amani iliyopo kwa kutangaza mambo mema yenye ukweli ndani yake badala ya kutangaza mabaya wanayoyasikia bila kujua ukweli uliopo.

" Ndugu zangu kuna mambo mengi ambayo Rais Magufuli ameyafanya ndani ya kipindi kifupi cha uongozi wake, zaidi ya vituo vya Afya 360 vimejengwa, Hospitali 62 Nchi nzima na mpaka kufikia mwakani tutakua tumekamilisha nyingine 20 tena za kisasa kwa ajili ya kuhudumia wananchi wetu wanyonge.

Kama hiyo haitoshi Rais Magufuli ameamua kusimamia sera ya elimu bure kwa vitendo, Shule karibia zote kongwe zimefanyiwa ukarabati mkubwa na zaidi amekua akitoa elimu bila malipo kuanzia Elimu ya Msingi hadi Kidato cha Nne, kwenye miundombinu ndio usiseme hivi mnataka watanzania tupewe nini zaidi? Niwaombe tuendele kushirikiana, " Amesema Mhe Jafo.

Aidha amezitaka Azaki hizo kutumia Taasisi zao kutoa kuhamasisha wananchi kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24 mwaka huu ili waweze kuwapata viongozi walio bora wenye kusimamia maslahi ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi Humphrey PolePole amesema
AZAKI na Serikali ni kitu kimoja hivyo haina haja ya kuogopana kama kuna suala lolote ambalo linapawa changamoto wasisite kushirikiana katika kukabiliana nalo na kulipatia ufumbuzi.

Nae Mkurugenzi wa Azaki nchini Francis Kiwanga amesema Azaki zipo kwa ajili ya kujenga na sio kubomoa kama baadhi ya watu wanavyofikiria na kuahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuleta maendeleo.

" Sisi tunaishukuru sana Serikali kwa kuendelea kutusapoti, mmekua na sisi kwa wiki nzima hapa Dodoma, viongozi wa kiserikali, Wabunge na wadau mbalimbali wameungana nasi katika kujadili maslahi mapana ya Taifa letu hasa katika ubia wa maendeleo, tuwaahidi kwamba Azaki itazidisha mapambano ya kuwakomboa watanzania kifikra ili kuweza kufikia lengo Kuu ifikapo 2020," Amesema Kiwanga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...