MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), imefanya ukaguzi katika vituo mbalimbali vya kutolea huduma za afya zikiwemo dawa na kugundua kuwepo kwa dawa bandia ambazo kwa sasa wanazishikilia.

Akizungumza leo Novemba 13,mwaka 2019 jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA,Akida Khea amesema kuwa katika kipindi cha kuanzia Julai hadi Septemba 2019, baadhi ya dawa bandia zilizobainika na kutolewa taarifa ya kuwepo katika nchi za wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ni pamoja na dawa aina ya Gentrisone Cream 10gm toleo namba GNTRO X030,Augmentin 625mg tables toleo namba 786627 na kapsuli za Cold caps.

"Viwanda halisi vinavyotengeneza dawa hizi vilithibitisha kuwa dawa hizo hazikutengenezwa na viwanda huzika,"amesema Khea. Aidha amesema kuwa kwa mujibu wa uchambuzi na uchunguzi uliofanywa na TMDA, matoleo ya dawa hizo husika yalithibitishwa kuwa ni bandia.

"Uchunguzi kupitia maabara ya TMDA kwa dawa ya Gentrisone cream 10gm toleo namba GNTRO XO30 ulionesha kuwa dawa hiyo haikuwa na viambato hai (active pharmaceutical ingrediets) vya dawa hiyo ambavyo ni Betamethasone Proprionate, Clotrimazole na Gentamycin sulfate,"amesema Khea.

Hata hivyo, Khea amesema kuwa katika operesheni ya ukaguzi katika Mikoa inayopakana na nchi za jirani ikiwemo mikoa ya Kigoma,Songwe,Kagera,Rukwa, Mbeya,Mara,Kilimanjaro, Arusha,Mwanza, Ruvuma,Mtwara na Tanga. Wakati mikoa mengine ni Dar es Salaam,Dodoma,Shinyanga,Geita,Singida ,Morogoro,Iringa, na Tabora

"Katika operesheni hii jumla ya maeneo 558 ikiwa ni famasi 209,maduka ya Dawa Muhimu 263, Vituo vya kutolea huduma za afya 27,Maduka ya Vifaa Tiba 21 na Vituo vya dawa asili na tiba mbadala 38 katika,"amesema Khea.
  Aina saba ya dawa duni na bandia zilizokamatwa katika ukaguzi maalum wa dawa ulioendeshwa na TMDA.
 Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo ya Teknolojia kutoka Wizara ya Mifugo na Uvivu,Chanasa Ngeleja akizungumza wakati wa uwasilishaji wa ripoti ya ukaguzi wa dawa leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka michuzi Tv)
aimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba (TMDA), Akida Khea akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) mapema wakati wa kutangaza matokeo ya ukaguzi maalum wa dawa vifaa tiba, vitendanishi, dawa asili na tiba mbadala, tukio lililofanyika makao makuu ya TMDA, Mabibo Jijini Dar e Salaam.

Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba (TMDA), Akida Khea akionesha moja ya dawa zilizokanatwa katika tukio hilo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema wakati wa kutangaza matokeo ya ukaguzi maalum wa dawa vifaa tiba, vitendanishi, dawa asili na tiba mbadala, tukio lililofanyika makao makuu ya TMDA, Mabibo Jijini Dar e Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...