Na Woinde Shizza Michuzi Tv

Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjin Patrobas Katabi ameingilia kati mgogoro wa mirathi wa watoto wa marehemu Hussein Bakari Dima wanainde otaka kudhulumiwa nyumba yao na ndugu wa marehemu baba yao iliyopo eneo la Kizota Area A Dodoma mjini.

Suala hilo ambalo lilianza takribani miezi miwili iyopita ambapo Shangazi na baba mdogo yao walikuja na hoja ya kutaka kuwakabidhi mali za urithi wa marehemu baba yao kwa kuwa watoto hao wamekwisha kuwa wakubwa na umri Zaidi ya miaka 18 na waweza kujitegemea.

Wakielezea sakata hilo watoto hao Omar Hussein (29) na Shamila Hussein (26)walitaka kufahamu mali ambazo shangazi yao anataka kuwakabidhi,lakini kinyume na matarajio yao shangazi yao alikuja na watoto wengine wawili akidai ni watoto wa nje ya ndoa wa marehemu ambao wanastahili kugaiwa nyumba hiyo ambayo tangu marehemu baba yao akiwa hai alishawarithisha.

“Sisi tulikataa ombi la shangazi ndipo alipoamua kwenda mahakamani kufungua ombi la kutaka kuwa msimamizi wa mirathi bila kutushirikisha wala kuwa na kikao cha familia ambacho kimemteua na kuwa na muhtasari wa kumkubalia kuwa msimamizi wa mirathi”.alisema Omary

Omar alisema baada ya shangazi kufungua kesi hiyo iliyosikilizwa kwa siku mbili na kutolewa hukumu licha ya kuwa hawajui sheria lakini hawakuridhishwa na uamuzi huo uliompa shangazi yao haki zote za kuwa msimamizi wa mirathi ikiwemo kuiuza nyumba yao na kumgaia mtoto anaeona anafaa au angependa.

“licha ya kumuomba Rais wetu Magufuli atusaidie tusidhulumiwe haki yetu tuliamua kwenda kwa mkuu wa wilaya kupeleka malalamiko yetu tukijua kuwa ndipo tunaweza kupata haki,kwa kuwa hatuna uwezo nwa kifedha na mahakamani hatujasikilizwa licha ya kuwa na hati halali za umiliki wa nyumba yetu, lakini hakimu alisema ni za kughushi bila kututhibitishia, shangazi ambae hakuwa na nyaraka yeyote alisikilizwa na kupewa haki ya kuwa msimamizi wa mirathi”Alisema Omary

Baada ya kupokea malalamiko ya watoto wa marehemu yaliyofikishwa kwa mkuu wa wilaya ya Dodoma yakionesha kutoridhishwa na uamuzi wa mahakama ya mwanzo ya Makole iliyotolewa Oktoba 28 na hakimu Nduka iliyompa mamlaka shangazi yao Zakhia Said kuwa msimamizi wa mirathi bila wao kusikilizwa watoto hao.

Omary alisema nyumba hiyo ilijengwa na baba na mama yao wakati wa uhai wao,ambapo baba yao alifariki mwaka 1998 na mama yao alifariki mwaka 2010, ambapo wamesisitiza kuwa tangu baba afariki hii nyumba ilikuwa chini ya umiliki weo wakisimamiwa na marehemu mama kwa kuwa tulikuwa bado wadogo ambapo wamemshangaa shangazi kuja na hoja ya kutaka kugawa mali za marehemu baada ya miaka 21.

Akizungumzia suala hilo mkuu wa wilaya ya Dodoma baada ya kufikishiwa malalamiko hayo na kuyapitia alitumia uamuzi wa kumuita shangazi yao afike katika ofisi yao ili kujua undani wa suala hilo ambapo alidai kuwa yupo mkoani Kilimanjaro.

Katabi amesema kwa namna alivyolitazama suala hilo alibaini kuwepo dosari nyingi za kisheria baada ya kuangalia mlolongo wote ameona kumekuwepo na ujanja ujanja baada ya kuangalia nyaraka zote.

“Hatua ya kwanza nimona niongee na hakimu mfawidhi ili aweze kuangalia mwenendo mzima wa shauri hilo jinsi ambavyo limeenda”alisema Katabi

Aliongeza kuwa wao kama serikali hawana wajibu wala haki ya kuingilia mahakama ila tuna haki ya kusimamia utaratibu,sheria kwa maana utawala wa sheria pale wanapoona kwamba kuna viashiria vya kupindishwa kwa sheria au kutokuwepo kwa misingi mizuri ya usimamizi wa sheria na haki hapo ndipo wanaingia kama sehemu ya serikali.

“nimefika hapa ili kwanza nilielewe eneo lakini pia kupata nyaraka hizo na pili kuwapta hao wanaolalamikiwa ili tuweze kupima na kuangalia haki iko wapi kwa hiyo tutafanya vizuri kabisa kwa kushirikiana na mahakama kuweza kuona haki ya watoto hawa inapatikana na awadhulumiwi.”alisema Katabi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...