Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar 08/12/2019

Mwenyekiti wa Kikundi cha Wanawake 15 ndani ya Muungano wa Jumuiya za Watu wanaoishi na Maradhi yasioambukiza Zanzibar (ZNCDA) Mwanakhamis Mohamed Abdalla ameiyomba Serikali kuzidisha juhudi kutoa elimu kwa wananchi juu ya kujikinga na maradhi yasioambukiza .

Ameyasema hayo huko Ofisini kwake kwa Bitihamrani Zanzibar wakati wa ufunguzi wa kikao cha kikundi hicho kwa waandishi wa habari jinsi ya msimamo baada ya kumaliza mafunzo yao juu ya umuhimu wa kujumuisha elimu,uchunguzi na tiba ya maradhi yasiyoambukiza katika mfumo wa afya .

Alisema hali ya maradhi yasioambukiza Zanzibar inazidi siku hadi siku hii inatokana kuwa wananchi kukosa uwelewa wa jinsi ngani ya kuyaepuka maradhi hayo.

Akiyaelezea maradhi hayo ni maradhi ya moyo,ugonjwa wa kisukari ,saratani pamoja na magonjwa sugu ya mfumo wa kupumua ambayo yanakadiriwa kusababisha vifo vya watu million 35 kila mwaka sawa na asilimia 60 ya vifo vyote ulimwenguni .

Aidha alisema Serikali kupitia Wizara ya Afya iendelee kutoa elimu kwa wananchi jinsi ya kuepuka maradhi yasioambukiza jambo ambalo linawezekana .

Nae Mjumbe wa Kukindi cha Wanawake hao Nunuu Kheir Saleh alisema kuengezeka kwa maradhi yasioambukiza ni moja kati ya changamoto za kiafya ambayo zinatishia maendeleo ya kiuchumi ,kijamii , maisha na afya ya mamilioni ya watu .

Alifahamisha tafiti zinaonyesha asilimia 80 ya vifo vinavyotokea katika nchi za kipato cha chini na cha kati husababishwa na maradhi hayo,ambayo yanauwezo wa kuepukika,ikiwemo maradhi ya moyo kiharusi kisukari cha aina ya 2 na saratani yanaweza kuzuilika kwa asilimia 80 iwapo jamii itakuwa tayari kujiepusha na tabia hatarishi ,

“Jamii ijiepusha na matumizi mabaya ya pombe,itumie vyakula vyenye lishe kamili ikiwemo matunda na mboga mboga , kufanye mazoezi kwa wingi waachane na matumizi ya tumbaku, “alisema Nunuu

Alisema kuwa shirika la afya ulimwenguni (WHO) linakadiria kuwa vifo vinavyotokana na maradhi yasioambukiza vitaongezeka kwa asilimia 17 ulimwenguni katika kipindi cha miaka 10 ijayo ikiwa hakuna hatua madhubuti zitakazochukuliwa .

Aidha alisema ongezeko kubwa la maradhi hayo litakuwa katika nchi za Afrika kwa asilimia 27 na Nchi za Mashariki ya Mediterania kwa asilimia 25. Vile vile Benki ya Dunia inatabiri kwamba vifo vitakavyotokana na maradhi yasioambukiza vimeongezeka kutoka asilimia 28 kwa mwaka 2008 hadi asilimia 46 ifikapo mwaka 2030 hali hii inawakilisha tishio kubwa kwa mifumo dhaifu ya afya na inasisitiza hitaji la njia bora za ubunifu katika utoaji wa huduma za afya.
Baadhi ya Waandishi wa Habari na Wageni waalikwa waliohudhuria katika mkutano kuelezea Umuhimu wa kujumuisha Elimu,Uchunguzi na Tiba ya Maradhi yasioambukiza(NCDs)katika mfumo wa Afya hafla iliofanyika katika ukumbi wa Ofisi hio kwa bitihamran Zanzibar. PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

Mwenyekiti wa Kikundi cha Wanawake 15 ndani ya Muungano wa Jumuiya za Watu wanaoishi na Maradhi yasioambukiza Zanzibar(ZNCDA)Mwanakhamisi Mohamed Abdalla akitoa maelezo ya makaribisho katika mkutano na Waandishi wa Habari kuelezea Umuhimu wa kujumuisha Elimu,Uchunguzi na Tiba ya Maradhi yasioambukiza(NCDs)katika mfumo wa Afya hafla iliofanyika katika ukumbi wa Ofisi hio kwa bitihamran Zanzibar.
Mjumbe wa kamati ya Maradhi yasioambukuza Nunuu Kheri Saleh akifafanua jambo wakati akitoa maelezo kwa waandishi wa Habari kuhusiana na Umuhimu wa kujumuisha Elimu,Uchunguzi na Tiba ya Maradhi yasioambukiza(NCDs)katika mfumo wa Afya hafla iliofanyika katika ukumbi wa Ofisi hio kwa bitihamran Zanzibar.
Mjumbe wa kamati ya Maradhi yasioambukuza Nunuu Kheri Saleh(wapili kulia ) akisoma maelezo kwa waandishi wa Habari kuhusiana na Umuhimu wa kujumuisha Elimu,Uchunguzi na Tiba ya Maradhi yasioambukiza(NCDs)katika mfumo wa Afya hafla iliofanyika katika ukumbi wa Ofisi hio kwa bitihamrani Zanzibar.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...