Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge amekutana na kufanya mazungumzo na Mabalozi mbalimbali wanaowakilisha nchi zao hapa nchini pamoja na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa tarehe 22 na 23 Januari 2020 katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine, mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia baina ya Tanzania na nchi hizo na mashirika hayo.
Mabalozi hao ni Balozi wa Visiwa vya Comoro, Mhe. Balozi Ahamada Elbadaour Mohamed, Balozi wa Ufaransa nchini, Mhe. Balozi Frederic Clavie, Balozi wa Denmark nchini Mhe. Balozi Mette Norgaard, Balozi wa Iran nchini, Mhe. Balozi Mousa Farhang, Balozi wa Ethiopia nchini, Mhe. Balozi Yonas Yosef Sanbe, pamoja na Balozi wa Italia nchini, Mhe. Balozi Roberto Mengoni.
Mbali na Mabalozi, Mkuu wa Itifaki, Balozi Kanali Ibuge amekutana na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa ambao ni Naibu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) Bw. James Gitau na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Aga Khan (AKDN) Bw. Amin Kurji.
Balozi wa Ufaransa nchini, Mhe. Balozi Frederic Clavie akimweleza jambo Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge wakati wa mazungumzo yaliyofanyika leo katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibugea kiongea na Balozi wa Ethiopia nchini, Mhe. Balozi Yonas Yosef Sanbe
|
Balozi wa Ethiopia nchini, Mhe. Balozi Yonas Yosef Sanbe akiongea na Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Wilbert Ibuge
|
Balozi wa Iran nchini, Mhe. Balozi Mousa Farhang akimsikiliza Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge wakati walipokutana kwa ajili ya mazungumzo leo katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
|
Balozi wa Italia nchini Meh. Balozi Roberto Mengoni akimsikiliza Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge wakati walipokutana kwa ajili ya mazungumzo leo katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge akiongea na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Aga Khan (AKDN) Bw. Amin Kurji
Naibu Rais wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) Bw. James Gitau, akiwa katika mazungumzo na Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge. Mazungumzo yaliyofanyika leo katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge akimfafanulia Naibu Rais wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) Bw. James Gitau wakati wa mazungumzo yaliyofanyika leo katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
|
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...