Mkuu wa Wilaya ya Tabora Komanya Kitwala ( wa pili kutoka kushoto) akisisitiza jambo jana wakati wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya Manispaa ya Tabora (DCC) cha kupitia makisio ya mapendekezo ya mpango na bajeti ya shilingi bilioni 52 kwa ajili ya mwaka wa fedha ujao wa fedha. 
Wajumbe wa Kamati ya Ushauri ya Manispaa ya Tabora (DCC) wakiwa katika kikao cha kupitia makisio ya mapendekezo ya mpango na bajeti ya shilingi bilioni 52 kwa ajili ya mwaka ujao wa fedha. 
Picha na Tiganya Vincent 







…………. 

NA TIGANYA VINCENT 

WAJUMBE wa Kamati ya Ushauri ya Manispaa ya Tabora (DCC) wamepitisha makisio ya mapendekezo ya mpango na bajeti ya shilingi bilioni 52 kwa ajili ya mwaka wa fedha ujao wa fedha. 

Wajumbe hao walipitisha mapendekezo hayo jana baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Tabora Bosco Ndunguru kuwasilisha wakati wa kikao kupitia mapendekezo ya bajeti ya mwaka 2020/21. 

Alisema katika mapendekezo hayo wanatarajiwa kukusanya shilingi bilioni 4.7 kutokana na mapato ya ndani ya Halmashauri ikiwa ni ongezeko la asilimia moja ukilinganisha na masikio ya mwaka 2019/20 ya kukusanya bilioni 4.6. 

Ndunguru alisema kwa upande wa Serikali Kuu na kwa wahisani wanatarajia kupata jumla shilingi bilioni 48 ikiwa ni ongezeko la asilimia 25 ukilinganisha na bilioni 38.2 ya mwaka 2019/20. 

Alivitaja vipaumbele vya bajeti ijayo kuwa ni uendelezaji wa jengo la utawala ambalo limetengewa milioni 200, kutenga fedha milioni 70 kwa ajili ya ununuzi wa ardhi ekari 140 za uwekezaji. 

Nduguru aliongeza kuwa vipaumbele vingine ni kutenga milioni 50 kwa ajili ya fidia kwa wananchi ili kutatua migogoro, milioni 84 kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya Shule za Msingi na Sekondari na ununuzi wa taulo kwa ajili ya wanafunzi wa kike na milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa Shule mbili za Kidato cha Tano na Sita. 

Aliongeza kuwa kiasi cha milioni 445 kinatarajiwa kutolewa kama mikopo ya vikundi vya vijana , wanawake na walemavu na milioni 117 zimetengwa kwa ajili ya shughuli za lishe. 

Ndunguru alisema kwa upande wa miradi wamependekeza shilingi milioni 580 zitumike katika miradi ya maendeleo kwenye Kata 29 za Manispaa ya Tabora na bilioni 1 zimetengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya Halmashauri hiyo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...