Katibu Mkuu
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
anayeshugulikia Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akizungumza na wadau
wa Sekta ya ajira kutoka Sekata za umma, binafsi na Mashirika Yasiyo ya
Kiserikali wakati akifungua jukwaa la majadiliano la wadau kuhusu utekelezaji wa dhana ya uanagenzi leo jijini Mbeya.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya
Mariam Mtunguja akiwasisitiza waajiri wa mkoa wa Mbeya na Mikoa ya
Nyanda za Juu Kusini kuwapokea wanafunzi na wahitimu wa vyuo vikuu kwa
mafunzo ya uanagenzi wakati wa jukwaa la majadiliano la wadau kuhusu
utekelezaji wa dhana ya uanagenzi liliofanyika leo jijini Mbeya.
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Patrick Golwike akifafanua jambo katika jukwaa la majadiliano la wadau kuhusu utekelezaji wa dhana ya uanagenzi lililofanyika leo jijini Mbeya.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Mbinga Juma Mnwele akichangia mada katika jukwaa la
majadiliano la wadau kuhusu utekelezaji wa dhana ya uanagenzi
liliofanyika leo jijini Mbeya.
Baadhi ya waajiri
kutoka Sekta ya Umma, Binafsi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutoka
mikoa ya Nyanda za Juu Kusini wakisikiliza mada mbalimbali zilizokuwa
zinazatolewa katika jukwaa la majadiliano la wadau kuhusu utekelezaji wa
dhana ya uanagenzi liliofanyika leo jijini Mbeya.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
*********************************
Na Mwandishi Wetu Mbeya
Katibu Mkuu
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
anayeshugulikia Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amesema kuwa dhana
Uanagenzi ni suluhisho la kuhakikisha mifumo yetu ya elimu inazalisha
wataalamu mahiri wenye ujuzi au stadi zinazohitajika katika soko la
ajira kwenye uchumi wa viwanda.
Dkt. Jingu
amesema hayo leo jiji ni Mbeya wakati wa akifungua Jukwaa la majadiliano
la wadau kuhusu utekelezaji wa dhana ya uanagenzi lililofanyika katika
ukumbi wa Benjamin Mkapa mkoani Mbeya.
Dkt. Jingu
amesema kuwa Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt John Joseph Pombe Magufuli imedhamiria kuwa
na nchi yenye uchumi wa kati wa viwanda kufikia mwaka 2025 na ujenzi wa
Tanzania ya viwanda unahitaji waajiriwa wenye stadi zinazohitajika na
soko la ajira kwenye sekta isiyo rasmi na rasmi.
“Hali ilivyo sasa
kuna tofauti kubwa kati elimu wanayopatiwa wahitimu wa fani mbali mbali
nchini na ujuzi au stadi zinazohitajika na soko la ajira alisema Dkt.
Jingu
Ameongeza
kuwa Serikali imeona umuhimu wa kushughulikia changamoto ya kuzalisha
wahitimu wasioajirika kwenye sekta rasmi na isiyo rasmi kwa kuanzisha
dhana ya uanagenzi kwenye Taasisi na vyuo vya Maendeleo ya Jamii
itakayosaidia kupata wataalam wenye ubora unaohitajika.
Dkt. Jingu
amesisitiza kupitia Mifano ya nchi za Ujerumani na Rwanda ikionesha kuwa
uanagenzi umewezesha kutoa matokeo chanya na Ujerumani waliingiza dhana
hii katika mfumo wa elimu ambapo imesaidia asilimia 60 ya wanafunzi
wanaomaliza vyuo kuweza kujiajiri wenyewe kutokana na ujuzi na uzoefu wa
kazi wanaoupata wakiwa masomoni kwa kupitia njia hiyo.
Akielezea dhumuni
la Jukwaa la majadiliano la wadau kuhusu utekelezaji wa dhana ya
uanagenzi Mkurugenzi Msaidizi Vyuo vya Maendeleo ya Jami Neema Ndoboka
amesema kuwa lengo kuu ni kuangalia namna ya kuboresha mafunzo kwa
vitendo na utekelezaji wa dhana ya uanagenzi katika kuhakikisha
wanafunzi na wahitimu wanapata stadi zinazohitajika katika soko la
ajira.
Ameongeza kuwa
katika kuelekea katika uchumi wa kati wahitimu wa vyuo wanahitajika kama
nguvu kazi katika kufikia hilo hivyo Serikali kwa kushirikiana na wadau
wa ajira wanajukumu kubwa la kuandaa nguvu kazi hiyo iliyo na weledi na
ufanisi katika kutekeleza majukumu yao.
Akitoa salamu za
mkoa wa Mbeya, Katibu Tawala wa Mkoa huo Mariam Mtunguja amewasisitiza
waajiri wa mkoa huo na Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kuwapokea wanafunzi
na wahitimu wa vyuo vikuu hasa vyuo vya Maendeleo ya Jamii nchini ili
waweze kupata ujuzi utakaowasaidia kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi
pale watakapoajiriwa na kujiajiri.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Juma Mnwele amesema kuwa
msisitizo uwekwe kwa Serikali kutoa muongozo kwa Taasisi za Serikali
kuwapokea wanafunzi kwa mafunzo kwa vitendo hasa ya uanagenzi katika
Taasisi za Serikali.
Naye Mwakilishi
wa Shirika la TAHEA Petre Mapunda amesema kuwa Shirkla lake linatekeleza
dhana ya uanagenzi kwa kuwapokea wanafunzi na wahitimu wa vyuo
mbalimbali katika Shirika lao kwa kufanya kazi kwa muda mrefu na
kuwezesha kupata ujuzi na kupata fursa za kuajiriwa na kujiajiri
kutokana na ujuzi walioupata.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...