.Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kaskazini (KCMC) Dkt.Sarah Urasa akizungumza na
waandishi wa habari na Timu ya Maafisa Habari na Uhusiano wa Taasisi 17 zilizo
chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto waliotembelea
hospitali hiyo kuangalia mafanikio ya miaka ya minne ya serikali ya awamu ya
tano ikiwa ni Kampeni ya Tumeboresha Sekta ya Afya .
Mkuu wa Msafara na Mkuu wa
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Gelald Chami akitoa maelezo kuhusiana na Kampeni ya
Tumeboresha Sekta ya Afya kutembelea kuona mafanikio ya miaka minne ya serikali
ya awamu ya tano.
Daktari Bingwa wa Uzazi wa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kaskazini (KCMC )
Benjamin Shayo akieleza kuhusiana uhifadhi ya mbegu za kiume kwa ajili ya watu
wenye tatizo la uzazi namna walivyofanikiwa mara baada ya kuuza kutoa huduma
hiyo.
Sehemu ya Mitungi ya Gesi ya Oksijeni ambayo inazalishwa Hospitali ya
Rufaa Kanda ya Kaskazini (KCMC).
Fundi wa Vifaa vya Tiba Dustan
Kanza akizungumza na waandishi wa habari namna wanavyofua hewa ya oksijen
katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kaskazini (KCMC)
Fundi wa Viti Mwendo wa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kaskazini (KCMC)
Prosper Kaaya akionesha namna wanavyotengeza viti vya magarudumu matatu kwa
ajili ya watu wenye ulemavu.
Mtaalam wa Afya wa Viungo Bandia
wa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kaskazini (KCMC) Sunday Agger akionesha namna wanavyounda viungo Bandia
katika hospitali hiyo.
Mfamasia wa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kaskazini (KCMC) Faustine Sasi akionesha waandishi wa habari namana
wanavyongeza maji tiba katika hospitali hiyo.
.Moja ya Viungo Bandia
vinavyozalishwa na hospatali Hospitali
ya Rufaa Kanda ya Kaskazini (KCMC).
picha ya mtoto aliyeunganishiwa
mguu wa bandia ulioundwa na Hospitali ya Rufaa kanda ya Kaskazini (KCMC)
Picha ya pamoja ya waandishi
habari na Timu ya Maafisa Habari na Uhusiano wa Taasisi 17 zilizo chini ya
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto watendaji Hospitali
ya Rufaa Kanda ya Kaskazini (KCMC).
*KCMC wanazalisha Hewa ya
Oksjeni kwa watu wenye matatizo ya
kupumua
Na Chalila Kibuda Globu ya Jamii,
Kilimanjaro
Katika kipindi cha Miaka Minne ya
utawala wa Rais Dkt.John Pombe Magufuli Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kaskazini
(KCMC) imefanya hospitali hiyo kuwa Hospitali ya Viwanda kwa kuzalisha Vifaa
tiba na Dawa kutokana uwekezaji wa miundombinu.
Katika Miaka Minne hiyo wameweza
kufanikiwa katika kuabzisha Kinu cha kufua hewa ya Oksijen na Nitrojen,Mafuta
ya Ngozi kwa watu wenye Ualbinino,Huduma ya magonjwa ya moja na kuunda
baskeli ya magurudumu Matatu, Kutengeneza maji tiba ‘DRIP’pamoja kuunda
viungo bandia bandia.
Kinu cha kuzalisha Oksijeni na
Naitrojeni kinauwezo wa kufua hewa ya
oksijeni ambayo kwa kiwango kikubwa hutumika kuwasaidia watu wenye matatizo ya
kupumua ambapo kwa siku wanazalisha mitungi 400 hufuliwa katika kinu hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari na Timu ya Maafisa
Habari na Uhusiano wa Taasisi 17 zilizo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto , Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kaskazini (KCMC) , Dkt.
Sarah Urasa amesema kuwa mafanikio walioyapata hayo wameweza kutoa huduma kwa
bora za matibabu kwa wananchi.
Amesema hospitali hiyo ni ya kwanza kuwa na kinu ya kufua hewa ya oksijeni
na Nitrogen hapa nchini,hewa ya oksijeni pia inatumika kwa wale wagonjwa
wanaopewa dawa za usingizi kwaajili ya upasuaji ,hewa ya nitrogen inatumika
kuhifadhi sampuli kutoka kwa wagonjwa,tiba kwa magonjwa ya ngozi vile vile
hutumika kukata matokeo kwenye ngozi au kwenye viungo vya uzazi"alisema.
Dkt.Urasa amesema ununuzi wa mitungi ya gesi ya oksijeni
pekee ulikuwa inaigharimu Hospitali zaidi
ya sh. milioni tatu kwa wiki hatua ambayo imeokoa gaharama za uendeshaji
hospitalini hapo na fedha iliyookolewa inafanya masuala mengine ya hospitali na
kuongeza kuwa kadiri uzalishaji
unavyoongezeka katika kinu hicho wataanza kutumia mfumo wa kuunganisha gesi
moja kwa moja hadi kwenda kitanda cha mgonjwa.
Amesema wameanza kuhifadhi mbegu za kiume kwa watu
wenye matatizo ya uzazi ambayo huwahudumia wagonjwa kwa wiki mara moja
ambapo huwahudumia watu 10 mpaka 12 kwa siku na wajo mbioni kuanzisha
kliniki kwa wiki mara mmoja kwa watu wenye matatizo hayo.
Dkt.Urasa alisema katika Utawala wa Rais Dkt.John
Magufuli wamefanikiwa kuanza kutengeneza maji tiba 'dripu' kwaajili ya
kuwasaidia wagonjwa ndani na nje ya hospitali na kusaidia kiwango kikubwa hata
hospitali zingine zimekuwa zikifika hapa kwaajili ua kujifunza namna ya
kutengeneza maji tiba
Pia amesema KCMC ndio kituo pekee
inayotambulika kimaitafa kutoa mafunzo ya magonjwa ya ngozi na zinaa kwa nchi
zote za Afrika Mashariki ambapo KCMC ndio Kituo hikinachozalisha mafuta ya
ngozi kwaajili ya watu wenye ualbino na tayari wameingia makubaliano na Bohari
kuu ya Dawa (MSD) kwaajili ya kusambaza mafuta hayo tayari wamefikia mikoa 25 kwa
kutumia mfumo wetu wa usambazaji na sasa MSD watatuongezea nguvu ili kusambazwa
nchi mzima "alisema
Akizungumzia matumizi ya mitungi ya
gesi kwa mgonjwa Mhandisi KCMC Dustan
Kanza alisema kwa wa mgonjwa mmoja hutumia mtungi mmoja lengo kuepukana na
maambukizi na kuongeza kuwa kinu hicho kwa saa 24 inauwezo wa kuzalisha mitungi
400 na mpaka sasa tayari zaidi ya mitungi 600 imezalishwa tangu kuanza kufanya
kazi kwa kinu hicho januari mwaka huu.
Kwa upande wake Meneja Uzalishaji
kitengo Idara ya ngozi Ebeneza Fabian alisema wanawafikia watu 6500 wenye
mahitaji ya dawa za ngozi huku idadi ya watu wenye ualbino ikiwa takriban
25,000 akitaja changamoto kuwa ni upatikaji wa malighafi ya kutengenezea mafuta
hayo na Mafunzo ya ufuaji wa gesi hizo zimesimamiwa na mtaalamu kutoka Nchini
India ikiwa ndio wauzaji wa mitambo hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...