Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
MSANII Godfrey Tumaini alimaarufu kama Dudubaya, amefutiwa usajili wa kutojuhusisha na shughuli zozote za sanaa hapa nchini kuanzia leo (Januari 7, 2020).

Hayo yameelewa katika taarifa iliyotolewa na katibu mtendaji wa Baraza la sanaa la Taifa(BASATA), Godfrey Mngereza leo jijini Dar es Salaam.

Hatua hiyo imechukuliwa na Baraza la sanaa la Taifa (BASATA)  baada ya kukataa wito ambao baraza hilo lilimtaka kufika katika ofisi zake zilizopo Ilala Sharif Shamba jijijini Dar es Salaam.

Msaanii huyo aliitwa na BASATA kutokana na alichokizungumza kuhusiana na wasanii na sekta ya sanaa kupitia mitandao ya kijamii kwa makusudi amekaidi wito huo.

Hata hivyo BASATA imesema kuwa haiwezi kuvumilia wasanii wachache wanaotaka kuigeuza sekta ya sanaa, kwa kutumia maneno yasiyo ya staha na Lugha chafu mbele ya jamii.

“BASATA haita kuvumilia wasanii wachache wanaotaka kuigeuza sekta ya sanaa kwa kutumia maneno yasiyo na staha na Lugha chafu mbele kwa jamii.”

BASATA imetoa onyo kwa taasisi, kampuni na mtu yeyote kutokufanya kazi na msaanii huyo kwani amekaidi agizo la baraza linaloshughulikia masuala ya sanaa na wasanii hapa nchini.

Baraza linawakumbusha wasanii na wadau wote wa sanaa nchini kufanya kazi kwa weredi kwa kuzingatia sheria, kanuni taratibu na miongozo inayosimamia sekta ya sanaa nchini pamoja na kuzingatia sheria za nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...