Na Chalila Kibuda,Michuzi Globu.

HOSPITALI ya Rufaa Mwananyamala imepata mafanikio katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya tano katika kuongeza ufanisi wa huduma katika kuhudumia wagonjwa mbalimbali wanapofika katika hospitali hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari pamoja na Timu ya Maafisa Habari wa Taasisi 17 zilizochini ya Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii , Jinsia ,Wazee na watoto Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Mussa Wambura amesema kuwa miaka mitano iliyopita walikuwa wanatoa huduma za kibigwa nne lakini sasa wanatoa 10 kutokana na kuwepo kwa rasilimali ya watumishi n mashine pamoja na miundombinu

Amese ma kuwa huduma za kibingwa zilizoongezeka katika kipindi cha miaka minne ni Mifupa, Mionzi ,Ngozi ,Meno pamoja na huduma za uchunguzi wa magonjwa hali ambayo imefanya hospatali hiyo kuwa ya sita wakati wizara ya afya,maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto walipofanya tathimini ya utaoaji huduma katika hospitali za serikali nchini.

Amesema kuwa wagonjwa wanaowaona kwa siku ni 1700 hadi 2500 ambao wote wanaofika hapo wanapata huduma kutokana na vifaa vilivyopo pamoja na upatikanaji wa dawa uliopo kwa asiliamia 97 hali mabayo ni tofauti na miaka mitano iliyopita wagonjwa wengi walikuwa wanatoa rufaa katika hospitali ya taifa Muhimbili.

Wambura amesema kuwa wanavyumba vinne vya upasuaji wakati awali walikuwa na vyumba viwili hivyo kumeongeza ufanisi wa watoaji huduma za upasuaji kuweza kufanyika kwa wagonjwa wanne kwa mara moja.

Aidha amemesema kuwa wamepunguza vifo vya mama na mtoto kutoka asilimia 17 hadi kufikia asilimia 12 huku jitihada zikifanyika za mahususi ya kuendeleoa kupunguza vifo hivyo kwa namba moja (single Diginit)

Amesema kuwa wanajengo la ghorofa tano ambapo litatumika kwa ajili ya mama na mtoto ambalo litakuwa la kisasa na vifaa vyote vitavyotumika katika jengo hilo tayari wameshaagiza ikiwa ni pamoja na jengo la TCCAN ambayo itafungwa muda mfupi katika hospitali hiyo na wana Utra Sound Tano ambapo kubwa ni tatu nan dogo mbili .

Katika Hospitali ya mwananyamala hawakuna takataka zinazotupwa kuanzi chupa za maji ya drip zinayeyushwa na kuuza pamoja kuchukua makondo ya akana mama wanaojifungua kutengenezea Biogas kwa ajili ya kuchemushia maji ya hospatali.

.Jongo la ghorofa tano linalojengwa kwa ajili ya mama na mtoto katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala .
Msanifu wa Majenzi wa Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii , Jinsia ,Wazee na watoto Abdulkarim Msuya akizungumza na waandishi habari kuhusiana na ujenzi wa jengo la mama na mtoto ambalo limefikia ujenzi asilimia 60 na linatarajiwa kukamilika mwezi wa Nne.
sehemu ambayo wanategeneza Gesi asilia kwa ajili ya kuchemshia maji yanayotokana na makondo ya akina mama waliojifungua katika hospitali hiyo ambapo Mwananyamala ndio ya kwanza kufanya hivyo.
Sehemu ya kuchomea takatataka za chupa baada ya hapo wanauza na fedha inaingia katika hospitali.
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Hospitali ya Mwananyamala Isdory Kiwale akionesha namna ya chumba cha kujifunzia kwa ajili ya mama ya mtoto namna ya utoaji huduma kwa mtoto.



Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufa ya Mkoa Mwananyamala Mussa Wambura akizungumza waandishi wa habari pamoja na Timu ya Maafisa Habari wa Taasisi 17 zilizo chini ya Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii , Jinsia ,Wazee na watoto wakati walipofika katika hospitali hiyo kuona mafanikio ya miaka minne ya Serikali ya awmu ya tano katika sekta ya afya kwa kampeni ya maafisa habari tUmeboresha sekta ya Afya .
Kaimu Mkuu wa Msafara wa Maafisa Habari wa Taasisi 17 zilizo chini ya Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii , Jinsia ,Wazee na watoto Siliveter Omary akitoa maelezo kuhusiana na kampeni ya Tumeboresha sekta ya afya kwa kipindi cha miaka minne ya serikali ya awamu ya tano .

Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Hospitali ya Mwananyamala Isdory Kiwale akitoa maelezo kuhusiana na maboresho mbalimbali katika hospitali hiyo na namna walivyoweza kwenda kwa kasi kwa kipindi cha miaka minne wakati Msafara wa Maafisa Habari wa Taasisi 17 zilizo chini ya Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii , Jinsia ,Wazee na Watoto pamoja waandishi walipofika katika hospitali hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...