Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima alipofanya ziara kwenye mradi wa
ujenzi wa kiwanda kipya cha bidhaa za ngozi cha Karanga (Karanga Leather Industries Company Limited (KLICL)
kilichopo katika Gereza la Karanga, Mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Anayetoa ufafanuzi ni Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho, Mhandisi
Masud Omari.
………………
Na Mwandishi Wetu, MOHA
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima, ameutaka uongozi wa Jeshi la
Magereza nchini, kutekeleza kwa wakati maelekezo yanayotolewa.
Pia amelitaka jeshi hilo litimize wajibu walionao pamoja na kujitathmini juu ya ujenzi wa miradi mbalimbali.Kailima aliyasema hayo jijini
Moshi, mkoani Kilimanjaro jana baada ya kukagua utekelezaji wa mradi wa
ujenzi wa kiwanda kipya cha bidhaa za ngozi cha Karanga (Karanga Leather Industries Company Limited (KLICL).
Mradi huo unahusisha ujenzi wa
majengo manne ambayo ni Cutting and stitching building, Lasting
building, Warehouse pamoja na Power house.
Ujenzi wa majengo hayo ulianza rasmi Oktoba 28,2019 ukitarajiwa kukamilika Februari 2, mwaka huu.
Katika ziara hiyo, Kailima
aliutaka uongozi wa jeshi hilo kutekeleza maelekezo yaliyotolewa na
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana, Wenye Ulemavu,
Andrew Massawe baada ya kukagua ujenzi huo.
“Nataka mtoa taarifa kwa wakati na
usahihi katika hatua zote za ujenzi, taarifa ni muhimu kwa utekelezaji
wa kazi ambazo zinafanyika kwenye mradi,” alisisitiza Kailima.
Awali Mkandarasi wa mradi kutoka
Prisons Corporation Sole, Mhandisi SP Julius Sukambi, alitoa taarifa
inayohusu maendeleo ya mradi huo akifafanua kuwa, ujenzi unafanyika
usiku, mchana.
Alisema nguvu kazi ya wafungwa 170 hushiriki ujenzi huo kuanzia asubuhi hadi jioni, wafungwa 50 huingia jioni hadi asubuhi.Pia jeshi hilo limeongeza nguvu
kazi ya wataalam wakiwemo Wahandisi wanne waliopo eneo la mradi,
kuongeza wasaidizi wa Wahandisi (technicians) na kufikia wanane.
“Sambamba na hilo, pia tumeongeza
mafunzi wa fani mbalimbali, kwa siku tuna mafunzi wasiopungua 100,
jitihada za kuongeza watendaji zimefanyika ili kukamilisha ujenzi kwa
wakati.“Kazi kubwa iliyokuwa inatukabili
ya ujenzi wa msingi imekamilika kwa asilimia 95 hivyo tunaamini kazi
zilizobaki zitakamilika kwa wakati,” alifafanua SP Sukambi.
Alisema tayari njia ya kuingia
eneo la mradi imetengenezwa, mabati ya kuezekea jengo la kupokea mitambo
yamepatikana ndani ya siku saba badaya ya 14, jengo limeanza kuezekwa.Akizungumzia changamoto, alisema
ni upatikanaji wa vifaa hasa mvua zinaponyesha vinavyotokana na madini
ya ujenzi kama mchanga, mawe, kokoto ambavyo havipatikani kwa urahisi
kutokana na magari kushindwa kuingia katika machimbo.
“Kazi zinaendelea kufanyika kwa
ufanisi na ubora zaidi, mashine, mitambo ya kiwanda tayari imewasiri
Bandari ya Dar es Salaam vikiwa katika ukaguzi kabla ya kuwasirishwa
kiwandani. “Mradi huu kwa asilimia 100
unasimamiwa na wazawa, Timu ya Mshauri mwekezaji wa mradi inashirikisha
TIRDO, Chuo cha Kikuu cha Dar es Salaam kitendo cha BICO pamoja na Chuo
Kikuu cha Ardhi kitengo cha ABECC.
Januari 15, mwaka huu, Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Ajira,
Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama alitembelea mradi huo.Katika ziara hiyo, Mhagama alisema
Serikali haijaridhika na kasi ya ujenzi wa kiwanda hicho kilichopo
kwenye Gereza la Karanga, kumtaka Mkandarasi akamilishe kazi kabla ya
Februari 2, 2020.
“Hakuna sababu ya mradi huu
unaotekelezwa kwa ubia kati ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi
wa Umma (PSSSF) na Gereza la Karanga kutokamilika kwa wakati.“Fedha zote zilizohitajika katika
hatua muhimu za mradi huo zimekwishatolewa, mradi huu ni miongoni mwa
miradi muhimu ya kimkakati iliyopangwa kutekelezwa na Serikali ya Awamu
ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli.
“Mkandarasi hana budi kuzingatia
masharti ya mkataba uliowekwa ili kuhakikisha kiwanda kinakamilika kwa
wakati ili kiweze kuleta tija iliyokusudiwa,” alisisitiza Mhagama.Aliuagiza uongozi wa jeshi hilo
kuhakikisha kunakuwepo vifaa, vitendea kazi na wataalamu wa kutosha
katika maeneo yote ya ujenzi ili uweze kukamilika kwa wakati.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...