Na Khadija Seif, Michuzi TV

WAKAZI wa Kata ya Msasani eno la bonde la mpunga wamelalamika baadhi ya wananchi ambao hawashiriki usafi kwenye mitaro ambayo imekua ikitiririsha maji machafu kutoka sehemu za kitongoji hicho.

Akizungumza na Michuzi TV mmoja wa wakazi wa bonde la mpunga Munira Abdallah ambae amekua akipata kadhia hiyo ya mafuriko kwa muda mrefu amesema tusilaumu Serikali wakati wote katika kuboresha miundombinu hasa mitaro.

"Serikali imekua ikijitahidi kuboresha miundombinu kuanzia kutengeneza makaravati yakutosha ambayo yanaruhusu  maji machafu kupitia na kuelekea moja kwa moja baharini kwenye mkondo wake lakini wananchi bado wamekua wakitupa takataka na kusababisha kuziba kwa karavati hizo na matokeo yake maji kuwa na nguvu na kuingia majumbani ,,"

Hata hivyo Mjumbe wa nyumba kumi Aziza Mwaimu amesema wakati mwengine wananchi wafanye usafi kwenye karavati pamoja na mitaro ili kuepuka kadhia ya mafuriko.

"Mitaro inapokua misafi hata maji unakuta hayasimami Tena au kurudi kwa kasi majumbani kwani kitendo Cha maji kurudi majumbani na kutuama sehemu moja yanasababisha magonjwa ya mlipuko na kupeleka kudhorota kwa shughuli za kijamii,"

Pia Mwaimu amewataka wakazi wawe walinzi kwa wenzao pindi wanapotupa taka kipindi cha mvua pamoja kufungilia uchafu wa kutokana vyooni.
 Moja ya nyumba ikiwa imejaa maji ndano kutokana na athari za mvua iliyonyesha leo Alfajiri katika eneo la  bonde la mpunga kata ya Msasani jijini Dar es salaam
 Maji yakiwa yamezunguka nyumba zilizopo kwenye eneo la bonde la Mpunga Msasani jijini Dar es salaam.
Barabara ya kanisa la Galilaya Msasani inayotengenezwa ikiwa imejaa maji na kusababisha kusimamishwa kwa ukarabati kutokana na mvua iliyonyesha alfajiri ya leo jijini Dar es salaam .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...