Mwenyekiti wa Baraza la Kilimo Dk.Jacline Mkindi (aliyevaa gauni rangi nyekundu) akikabidhi cheti kwa mkulima wa mazao ya kilimo hai.
Mkurugenzi wa Shirika la Floresta Richard Mhina (katikati) akielezea mikakati ya shirika hilo pamoja na kutaja majina ya vinara wa kilimo hai mkoani Kilimanjaro.
Wananchi wakiwa katika maonesho ya wakulima wakifuatilia hotuba zilizokuwa zinatolewa na wadau wa kilimo hai nchini




sehemu ya wananchi ambao ni wadau wa kilimo hai wakiwa katika maonesho ya wakulima yaliyofanyika Uwanja wa Ushirika mkoani Klimanjaro.Maonesho hayo yameandaliwa na Shirika la Floresta.



Na Said Mwishehe, Michuzi Globu ya jamii


WAKULIMA nchini wameshauriwa kujikita katika kilimo hai kwani mazao yatokanayo na kilimo hicho hatana madhara na ni salama kwa binadamu na hulinda afya ya mlaji.

Ushauri huo umetolewa na Mwenyekiti wa Baraza la Kilimo Tanzania Dk.Jacline Mkindi ambapo amefafanua asilimia kubwa ya vyakula vinavyoingia sokoni kutoka shambani vina sumu kutokana na aina ya kilimo kinachotumika kutumia kemikali nyingi za viwandani.

Akizungumza zaidi wakati wa maonesho ya wakulima wa bidhaa zinazotokana na kilimo hai yaliyofanyika viwanja vya Ushirika mkoani Kilimanjaro Dk.Mkindi amesema kuna kila sababu kwa jamii kuelekeza nguvu zao kwenye kilimo hai ili kupata chakula kilichokuwa salama kwa afya za mlaji.

Wakati wa maonesho zaidi ya wakulima 12,000 walishiriki na waandaji ni Shirika lisilo la kiserikali la Floresta Tanzania ambao ni sehemu ya mwanachama wa Shirika la Kuendeleza Kilimo hai Tanzania(TOAM).

"Utafiti unaonesha kasi ya vyakula vyenye sumu katika masoko ni kubwa. Ni wakati muafaka kwetu sote kuendelea juhudi za Floresta na wadau wengine wa kilimo kujikita kwenye kilimo hai ambacho kitatuhakikishia usalama wa afya zetu,"amesema Dk.Mkindi.

Mbali ya baraza hilo kusisitiza kilimo hai nchini, pia mwenyekiti huyo amesema wanao mpango wa kuanza kupima vyakula vyote vinavyouzwa katika soko la ndani kama ili kutambua ubora wake kama ilivyo kwenye soko la kimataifa.

"Uwepo wa vyakula vyenye sumu sokoni ni moja ya sababu ya kuongezeka magonjwa kama kisukari, saratani, moyo na mengine.Ni matumaini yetu ili kukabiliana na bidhaa zenye sumu wakulima tunayo sababu ya kujikita kwenye kilimo hai ambacho kinakubalika duniani kwa sasa,"Dk.Mkindi.

Ameongeza vyakula ambavyo vina sumu vimesababisha wawekezaji nchini kuagiza vyakula kutoka nje jambo ambalo sio jema kwa nchi huku akifafanua sekta ya madini nchini inaagiza asilimia 65 ya bidhaa za mboga na matunda zinatoka nchini Afrika Kusini, hivyo wakulima wanapswa kutumia fursa hiyo kuchukua soko.

Pia amewashauri wakulima kutumia fursa za biashara kimataifa na kikanda ili kujiinua kiuchumi na maendeleo.Sekta hiyo inakukua kwa kasi na sasa imefikia

asilimia 3.5 kwa mwaka huku mboga mboga na matunda ikifikia asilimia 12.Aidha mauzo ya mazoa yameondezeka hadi kufikia dola milioni 700 kutoka dola milioni 64, hivyo Tanzania ina fursa ya kuuza mazao yenye thamani ya dola bilioni 1.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Floresta Richard Mhina amesema shirika hilo limefanikiwa kuanzisha vikundi 450 ambavyo vinahusisha kundi kubwa la wananchi vijijini."Kila mwaka tunapanda miti milioni 1.5 na asilimia 70 inaota lengo ni kuifanya Kilimanjaro inakuwa na mazingira bora. Ila kilimo hai kimeweza kukomboa wakulima wengi," alisema.

Pia amesema Floresta limefanikisha wakulima kutambua masoko ya ndani na nje jambo ambalo linawaongezea mapato.Wakati wa maoesho hayo wakulima ambao wamefanya vizuri wamepata zawadi mbalimbali ikiwemo vyeti na mbuzi kama sehemu ya kuwahamasisha na kutambua mchango wao kwenye sekta ya kilimo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...