Anaandika Abdullatif Yunus  Michuzi TV.

Idara ya Uhamiaji Mkoani Kagera inawashikilia watu wawili mmoja akiwa ni Raia  kutoka nchini Uganda na Mtanzania mmoja kwa tuhuma za kughushi nyaraka za kujisajili ili kupatiwa kitambulisho cha Taifa, katika harakati za kufanikisha zoezi linaondelea hapa nchini la kukamilisha usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.

Kwa mujibu wa Kamishna msaidizi Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kagera ACI Pendo C. Buteng'e amesema Tukio hilo limetokea Mnamo Januari 06, 2019 likiwahusisha Watu wawili ambao amewataja kuwa ni Frank Mpuuga (Raia kutoka Uganda), ambae amekuwa akishirikiana na Mwenyeji wake  Mtanzania aitwae Swalehe Abasi Athumani Mkazi wa Mutukula Wilayani Missenyi, kughushi Nyaraka mbalimbali zikiwemo kitambulisho cha Taifa ili kuweza kukamilisha Usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.

Afande Buteng'e ameongeza kuwa kukamatwa kwa Watuhumiwa hao kumetokana na taarifa za kiiterenjesia zilizoonesha Mtuhumiwa Frank Mpuuga kuwa na cheti cha kiapo cha wakili, akiwa tayari amekwisha jisajili NIDA kwa jina tofauti, akiwa ameingia Nchini kwa kutumia Hati ya kusafiria ya Nchini Uganda, baada ya kuhojiwa amemtaja Swalehe Athumani (mkazi wa Mutukula) kuwa ndie aliyekuwa akishirikiana nae ili kuweza kufanikisha zoezi la Vitambulisho vya Taifa na usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.

Aidha Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti amewasihi Wanakagera waishio maeneo ya mipaka kuwafichua wale wote wanaotaka kughushi, na kufanya Udanganyifu wa aina yoyote ile ili kujipatia Vitambulisho, na kusisitiza hatua Kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao pamoja na  Raia kutoka Nchi za jirani kuzunguka Mkoa Kagera wanaoshirikiana nao akiongeza kuwa wathumiwa waliokamatwa  watakuwa mfano kwa wengine.
 Pichani ni watuhumiwa wanaoshikiliwa kwa makosa ya kugushi Vitambulisho na Nyaraka ili kusajili laini zao kwa alama za vidole, kushoto ni Mtanzania Swalehe Athumani mkazi wa Mutukula Upande wa Tanzania, na Frank Mpuuga Raia kutoka Mutukula Upande wa Uganda.
 Pichani ni Kamishna Msaidizi Idara ya Uhamiaji Mkoani Kagera ACI Pendo Buteng'e akitoa Maelezo kwa Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti, aliyefika katika Ofisi za Uhamiaji kutaka kufahamu namna zoezi la uthibitisho wa Uraia linavyoendelea katika kufanikisha zoezi la usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.

 Pichani Ni jengo la Ofisi za Uhamiaji na Magereza Mkoani Kagera, shughuli za kuthibitisha Wananchi ili waweze kusajiliwa na wengine kupata Vitambulisho pamoja na Hati za Kusafiria likiendelea mapema Januari 08,2019.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...