Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar
Waziri wa Biashara na Viwanda Balozi Amina Salum Ali amesema ushindani wa bidhaa nchini  unahitaji  mpangilio  maalum unaotokana na sera, sheria pamoja na soko la uuzwaji wa bidhaa hizo .

 Hayo ameyasema wakati akifungua Mkutano wa Wajasiriamali kuhusiano na Mpango wa kuhimili ushindani wa kibiashara  nchini huko katika Hoteli ya Verde Maruhubi .

Alisema ushindani wa biashara unahitaji mpangilio kwa kutoa mafunzo ya uzalishaji wa bidhaa kwa wajasiriamali ili kuweza kufuata maadili  ya wataalamu kwa kukuza uzalishaji na kuongeza kipato kwa wafanyabiashara wadogo wadogo.

Alisema kuwa wajasiriamali wa bidhaa ya mwani wameweza kupatiwa mafunzo ya mwani wa aina mpya ambayo unauwezo wa kutoa mbegu ya mwani kwa wingi hadi mashamba  kuimarika na kuongezeka kwa uzalishaji wa bidhaa hiyo .

Aidha alisema Wajasiriamali waliopata mafunzo kwa upande wa Pemba ni katika Kijiji cha Makangale ,Tumbe ,Chokocho pamoja na Kusini, Kaskazini na Magharibi kwa Upande wa Unguja .

Alifahamisha kuwa changamoto zilizopo kwa wasiriamali hao ni ukosefu wa baadhi ya vifaa vya kufanyia kazi pamoja na boti ya uokozi pia wanahitaji  mafunzo ya uokoaji na upigaji mbizi  .

Alisema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar tayari imeshatiliana Mkataba katika Kampuni mbili tofauti pamoja na Utayarishaji wa ujenzi wa kiwanda cha mwani.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Repoa  Dr.Donald Mmari amesema wamekuwa wakishughulikia sera ya masoko ya ndani na ya nje ya bidhaa mbali mbali ikiwemo bidhaa za mbogamboga ngozi pamoja na zao la  mpunga kwa lengo la kuimarisha bidhaa hizo ili ziweze kuingia katika ushindani wa kIbiashara .

Alifahamisha kuwa kwa upande wa bidhaa ya mwani huwasaidia kipato kwa wakulima wa mwani kutokana na kukuwa kwa uzalishaji wa bidhaa hiyo na kuweza kumiliki soko la ushindani

Alisema sera ya viwanda ina lengo la kukuza uzalishaji wa bidhaa kwa kukidhi mahitaji ya masoko pamoja na kuweza kuingia katika soko la ushindani .
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya kufanya Utafiti wa Uchumi na Sera (REPOA) Dkt,Donald Mmari akitoa hotuba ya makaribisho katika Mkutano  wa Taasisi ya Kufanya Utafiti wa Uchumi na Sera (REPOA)kuhusiana na Mpango wa  kuhimili Ushindani wa Kibiashara hafla ilofanyika Hoteli Verde Maruhubi Zanzibar.
 Waziri wa Biashara na Viwanda Balozi Amina Salum Ali akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Mkutano  wa Taasisi ya Kufanya Utafiti wa Uchumi na Sera (REPOA)kuhusiana na Mpango wa  kuhimili Ushindani wa Kibiashara hafla ilofanyika Hoteli Verde Maruhubi Zanzibar.
  Waziri wa Biashara na Viwanda Balozi Amina Salum Ali(Katikati)akiwa katika picha ya pamoja na Wadau na Viongozi  Katika Mkutano  wa Taasisi ya Kufanya Utafiti wa Uchumi na Sera (REPOA)kuhusiana na Mpango wa  kuhimili Ushindani wa Kibiashara hafla ilofanyika Hoteli Verde Maruhubi Zanzibar.
 Waziri wa Biashara na Viwanda Balozi Amina Salum Ali akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya ufunguzi wa  Mkutano  wa Taasisi ya Kufanya Utafiti wa Uchumi na Sera (REPOA)kuhusiana na Mpango wa  kuhimili Ushindani wa Kibiashara hafla ilofanyika Hoteli Verde Maruhubi Zanzibar.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya kufanya Utafiti wa Uchumi na Sera (REPOA) Dkt,Donald Mmari akizungumza na Waandishi wa Habari katika Mkutano  wa Taasisi ya Kufanya Utafiti wa Uchumi na Sera (REPOA)kuhusiana na Mpango wa  kuhimili Ushindani wa Kibiashara hafla ilofanyika Hoteli Verde Maruhubi Zanzibar.
Baadhi ya Wadau wa maswala ya Biashara waliohudhuria katika Mkutano wa Taasisi ya Kufanya Utafiti wa Uchumi na Sera (REPOA)kuhusiana na Mpango wa  kuhimili Ushindani wa Kibiashara hafla ilofanyika Hoteli Verde Maruhubi Zanzibar. PICHA NA YUSSUF SIMAI/-MAELEZO ZANZIBAR.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...