Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

NUNO Ribeiro da Cunha(45) ambaye ni ameelezwa kuhusika na kesi matumizi mabaya ya fedha dhidi ya mwanamke tajiri zaidi barani Afrika aliyetajwa na jarida la Forbes mapema mwaka huu amefariki dunia na kifo chake kuripotiwa jana na hiyo ni mara tuu baada ya waendesha mashtaka wa Angola kuwataja Isabela Dos Santos na Nuno kama washukiwa.

Imeelezwa kuwa Nuno ambaye pia ni mfanyakazi wa benki alikuwa msimamizi wa kampuni ya mafuta ya Sonangol na alipatikana amefariki mjini Lisbon huku taarifa za awali zikieleza kuwa huenda amejiua mara baada ya kushukiwa katika sakata hilo.

Mapema jumatano benki ya EuroBic ambayo Isabela alikuwa Mwenyekiti ilisema itasitisha uhusiano wa kibiashara pamoja na kuchunguza uhamisho wa fedha nyingi kutoka kwenye akaunti ya Isabela ambaye ni mwanahisa mkuu wa benki mkuu wa benki hiyo.

Licha ya Isabela kukana madai hayo gazeti la New York times limeripoti kuwa baadhi ya fedha hizo zilizoelezwa kuwa ni mamilioni ya madola ni baadhi ya fedha zilizofilisi akaunti ya Sonangol katika benki ya EuroBic.

Imeelezwa kuwa waendesha mashtaka wa Angola wanajaribu kuzinusuru dola za kimarekani bilioni moja ambazo Isabela na wadau wake wanadaiwa kuzichota kutoka katika taifa hilo.

Licha ya kutajwa katika orodha ya watu watano waliotakiwa kurudi nchini Angola, Ribeiro amejitoa uhai wake kama ilivyoelezwa, na Mamlaka zimeeleza kuwa ikiwa Isabela hatorudi kwa hiari basi agizo la Kimataifa la kumkamata litatolewa.

Isabela Dos Santos (46) ambaye ni mtoto wa aliyekuwa Rais  Jose Eduardo Dos Santos ambaye alitawala  miaka 38 amekumbana na kashfa ya ubadhilifu wa fedha kupitia mikataba ya sekta za ardhi, gesi, mafuta na madini mikataba ambayo ilipitishwa wakati wa utawala wa baba yake.

Isabela, mama wa watoto wawili na mume wa mfanyabiashara maarufu kutoka nchini Kongo mwenye makazi nchini Marekani alitangaza nia ya kugombea urais nchini humo alikana madai hayo na kueleza kuwa ni hizo ni vita vya kisiasa toka kwa serikali iliyopo dhidi yake ambapo hadi sasa malinzake zimeshikiliwa na mamlaka nchini Angola.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...