Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu wa Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Matias Haule akitoa ufafanuzi kuhusu maambukizi ya mapya ya UKIMWI kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Mininngani iliyoko Kondoa Mjini Mkoani Dodoma.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Miningani iliyoko nje kidogo ya mji wa Kondoa wakisiliza kwa amakini mafunzo ya maambukizi ya UKIMWI kwa Vijana jana Kondoa Mkoani Dodoma.
*******************************
Na mwandishi wetu Kondoa
Wazee Wilayani Kondoa wameiomba Serikali kudhibiti picha zenye maudhui ya ngono katika mitandao ya Kijamii kwa lengo la kusaidia kupunguza maambukizi mapya ya UKIMWI kwani picha hizo zisizo kuwa na maadili zinawachochea vijana  kujiingiza katika matendo yanayosababisha maambukizi ya UKIMWI.
Wazee hao waliyasema hayo wakati wa mafunzo ya Siku moja kwa wazee wa mila pamoja na viongozi wa dini yaliyoandaliwa na Wizara ya Afya Idara Kuu Maendelepo ya Jamii kwa lengo la kuwafundisha kuhusu  ukubwa watatizo la UKIMWI kwa vijana na kuwataka kusaidia kupambana na tatizo hilo katika jamii kupitia nafasi zao.
Mzee Mohamed Hussein Kola akitoa maoni yake katika kikao hicho alisema hata Siku mmoja hakuna mtu aliyefikishwa mbele ya sheria kwa mtu kuambukiza mwenzake UKIMWI kwa makusudi pamoja na uwepo wa sheria ya UKIMWI hapa Nchini.
Mzee Kola anaangazia pia suala la malezi na kusema kwamba vijana hawaeshimu tena mawazo ya wazee na kudai kuwa kila mzee akitoa maoni yake vijana wanasema mawazo ya mzee nayo yamepitwa na wakati na kudai kuwa hata kwa baadhi ya mafunzo ya magonjwa mbalimbali yanapotolewa wazee wamekuwa hawashirikishwi.
Mzee Haruna Ramadhani Dodi pia aliongeza kuwa vijana wadanganyana kupuuza uwepo wa maambukizi ya UKIMWI na kudai kuwa watakufa kishujaa uku akiwataka kupuuza mawazo haya kwani hakuna mtu aliyewai kufa kishujaa na kuonya pia juu ya uwepo wa maeneo ya biashara za kumbi za starehe kuwa zinachangia uwepo wa maambukizi. 
Taarifa hizi kwa wazee hao zilikuwa za kushtua kwani idadi ya maambukizi kwa vijana inazidi kupaa na hii ilizibitishwa na Afisa Maendeleo Mkuu kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Matias Haule aliyesema kuwa watanzania 200 wanapata maambukizi mapya kwa siku.
Aidha Bw. Haule alitoa takwimu hizo na kuongeza kuwa maabukizi haya kwa mwaka ni kiasi cha watu elfu 72 akiitaja idadi ya watu inayoambukizwa kwa mwezi kuwa watu elfu 6,000 na kushangaza wazee hao kwa kusema kwa vijana wenye umri kati ya miaka 15-24 maambukizi mapya kwao 79 na kati yao wasichana wanaombukizwa ni 63 hivyo idadi kubwa ya wasichana inaambukizwa ukilinganisha na wavulana.
Wizara ya Afya Maendealeo ya Jamii kwa Kushirikiana na TACAIDS pamoja na Shirika la TASAF wako Mkoani Dodoma kutembelea wasichana barehe na wanawake vijana pamoja na Shule mbalimbali Mkoani humo kwa lengo la kuhamasisha vijana juu yatishio jipya la maambukizi ya UKIMWI kwa vijana na zoezi hili litaendelea kwa Mkoa wa Morogoro na baadae Nchi Nzima.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...