Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imewapa mafunzo Wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA) mwaka wa kwanza, wa pili na wa tatu wanaochukua kozi ya Ununuzi na Ugavi.

Akizungumza na Michuzi  Blog, Kaimu Mkurugenzi wa mafunzo wa Bodi ya wataalumu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Amani Ngonyani amesema Bodi hiyo imeendelea kuwapa mafunzo Wanafunzi wa Vyuo mbalimbali wanaochukua kozi hiyo ya Ununuzi na Ugavi kuhusu shughuli zinazofanywa na Bodi hiyo, kuhusu Mitahani inayotungwa na Bodi, Usajili kwa njia ya mtandao na masuala ya ajira pamoja na  maadili na miiko

Ngonyani amesema  Wanafunzi hao wanekuwa na mwamko katika maada hizo kujifunza zaidi katika masuala hayo kuhusu masuala mbalimbali yanayofanywa na Bodi, Usajili na maadili kwa Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi.

"Wanafunzi wa mwaka wa kwanza wamekuwa na mwamko zaidi katika masuala haya yakujengewa uwezo na PSPTB", amesema Ngonyani.

Pia amesema PSPTB ina lengo kuvijengea uwezo Vyuo vingine mikoani kwa kutoa mafunzo katika masuala hayo, amesema wataenda Dodoma, Morogoro, Moshi, Mtwara pamoja na Mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Kaimu Mkurugenzi wa mafunzo wa Bodi ya wataalumu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Amani Ngonyani akiwasilisha mada kwa Wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA) mwaka wa kwanza, wa pili na wa tatu wanaochukua kozi ya Ununuzi na Ugavi wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyoandaliwa na Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB).
.Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Paul Bilabaye akitoa mada wanafunzi wa mwaka wa kwanza, wa pili na wa tatu wanaochukua kozi ya Ununuzi na Ugavi wa Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA) wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyoandaliwa na Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB).
Afisa TEHAMA kutoka Bodi ya wataalumu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Boniface Mushi akitoa mada kuhusu namna ya usajili unavyofanyika kupitia tovuti ya Bodi hiyo  kwa Wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA) mwaka wa kwanza, wa pili na wa tatu wanaochukua kozi ya Ununuzi na Ugavi wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyoandaliwa na Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB).
.Afisa Mwandamizi wa Masoko na Mahusiano ya Umma - PSPTB, Shamim Mdee akizungumza wakati mafunzo mada wanafunzi wa mwaka wa kwanza, wa pili na wa tatu wanaochukua kozi ya Ununuzi na Ugavi wa Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA) wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyoandaliwa na Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB).
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA) mwaka wa kwanza, wa pili na wa tatu wanaochukua kozi ya Ununuzi na Ugavi  wakichangia mada kwenye mafunzo yaliyoandaliwa na Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB)
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA) mwaka wa kwanza, wa pili na wa tatu wanaochukua kozi ya Ununuzi na Ugavi wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zinatolewa na wataalamu kutoka Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB)
Rais wa PSA, Ndikumana Nyarema akiwakaribisha wageni kutoka Bodi ya wataalumu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) pamoja na  Wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA) mwaka wa kwanza, wa pili na wa tatu wanaochukua kozi ya Ununuzi na Ugavi waliofika kwenye mafunzo hayo yaliyofanyika katika Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...