Na Said Mwishehe, Michuzi Globu ya jamii

RAIS John Magufuli amewawaapisha mabalozi wanne leo Januari 14, mwaka 2020 , Ikulu jijini Dar es Salaam huku akiwataka kuondoka nchini kwenda kwenye nchi ambazo wanatakiwa kwenda ambapo amewapa wiki moja wote wawe wameondoka nchini.

Amesema kumewepo na tabia ya baadhi ya malozi wanapopishwa badala ya kwenda kuwakilisha nchi na kuanza majukumu yao wanatumia muda mwingi kubaki nchini wakiaga kwa kupita ofisi moja baada ya nyingine, hivyo Rais amesema waliopishwa wanapaswa kuondoka na kuachana na tabia kuaga aga.

Mabalozi ambao wameapishwa leo ni Meja Jenerali Gaudence Milanzi ambaye anakwenda kuwa Balozi nchini Afrika Kusini, Dk Modestus Kipilimba anayekwenda kufungua ubalozi nchini Namibia, Mchungaji Profesa Emmanuel David anayekwenda nchini Zimbabwe na Dk.Benson Bana anakwenda nchini Nigeria na kuwakilisha vituo vingine 16 vya nchi za Magharibi.

Rais Magufuli baada ya kuwaapisha amewataka mabalozi hao kuondoka nchini na kisha kwenda kwenye nchi hizo kusimamia uchumi na kuhakikisha wanatengeneza ajira ya Watanzania katika nchi wanazowakilisha.

Rais Magufuli amewaambia hivi “Kasimamieni uchumi, kasimamieni taifa, kahakikisheni mnatengeneza ajira ya watanzania katika nchi mnazoziwakilisha ninajua mkienda kusimama vizuri mtafanya mazuri.

“Hapo mwanzoni kulijengeka tabia ya mabalozi wanapoteuliwa na kisha kuapishwa hawaendi sehemu zao za kazi hadi waage watumishi wenzao. Atakaa kuzunguka kila ofisi anakuja kuaga kwa Rais, anakwenda kwa Makamu wa Rais, anaenda kwa Waziri Mkuu, Waziri wa mambo ya nje, mwisho Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wengine wanaenda hadi kwa Wakurugenzi na wakuu wa Mikoa”.

Hivyo amesema kuwa mabolozi ambao wameapishwa ataomba barua zao zipelekwe mapema ili ikiwezekana ndani ya wiki moja wawe wameshaenda kwenye nchi hizo ambazo wanakwenda kutuwakilisha.

Ameongeza kwamba mabalozi wanapoteuliwa wanapaswa kufanya kazi ili kutekeleza kauli mbiu ya hapa kazi tu. “Tunataka unapoteuliwa uchape, kazi na ndiyo maana halisi ya Hapa Kazi Tu.Nchi ambazo walizowapeleka mabalozi hao ni nzuri katika kujenga uchumi wa taifa .”

Hata hivyo amesema kila nchi inaumuhimu wake hivyo kuteuliwa kwao na kutekeleza majukumu yao kuna faida kwa taifa kwa ujumla. “Waziri ameeleza Afrika kusini, Naminia, Zimbabwe zote ni wanachama wa SADC na mnafahamu mikakati ya wanachama tuliyonayo ya SADC katika kujenga maendeleo na uchumi wa kisasa.”

Awali akizungumza katika sherehe hizo za uapisho wa mabalozi hao,Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki nchini Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi amesema Tanzania ilizembea kupata fursa ya kufundisha lugha ya Kiswahili nchini Afrika Kusini na kusababisha fursa hiyo kuangukia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

“Juhudi za Rais Mahuguli alizofanya wakati akipofanya ziara nchini humo mwaka 2019 zimezembewa huku akimtaka Balozi mpya anayeiwakilisha Tanzania nchini humo, Meja Jenerali Gaudence Milanzi kutoipoteza tena fursa hiyo tena.Msema kweli ni mpenzi wa Mungu, fursa hiyo ilikuwa imetuteleza na ilikuwa imeangukia mahali ambapo kwa hadhara hii nisiiseme lakini mmoja anaifahamu,”amesema Profesa Kabudi.

Amesema kwa isingekuwa juhudi binafsi za Rais alipokutana na Rais wa Afrika Kusini bahati hiyo ilikuwa imetupita na kwamba awe mkweli, fursa hiyo ilikuwa imetupita si kwa sababu yoyote ile bali ni uzembe wetu wenyewe,”alisema.

Pia Profesa Kabudi amemtaka Meja Jenerali Milanzi kumtafuta Waziri wa Basic Education (elimu ya msingi) wa Afrika Kusini ili jambo hilo likamilishwe kabla ya Februari mwaka huu ili juhudi binafsi za Rais alipokutana na Rais Cyril Ramaphosa zisipotee. Tusifanye makosa mara ya pili kuipoteza fursa hiyo. Itakuwa muhali,” amesema.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...