Victory Masangu, Kisarawe
WAKINAMAMA wa kata ya Msanga Wilayani Kisarawe Mkoa wa Pwani waliokuwa wanakabiliwa na kilio cha muda mrefu cha kutembea umbali mrefu wa zaidi ya kilometa 15 kwa ajili ya kwenda kupatiwa matibabu katika maeneo mengine hatimaye wamepata mkombozi baada ya serikali ya awamu ya tano kutoa kiasi cha shilingi milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha afya ambacho kitasaidia kupunguza vifo vinavyotokea wakati wa kijifungua.

Hayo yalibainishwa na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za miko na serikali za mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo wakati wa ziara yake ya kikazi kwa wananchi wa Wilaya ya Kisarawe yenye lengo la kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo ikiwemo sekta ya afya na elimu sambamba na kuzungumza na kusikiliza kero na changamoto za wananchi ambapo ametoa muda wa miezi mitatu kwa uongozi wa halmashauri ya Kisarawe kukamilisha ujenzi huo ambao wa kituo cha afya.

Aidha Jafo alisema kwamba lengo kubwa la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha kwamba inaboresha sekta ya aafya katika maeneo mbali mbali ikiwemo kuimarisha miundombinu ya majengo pamoja na kuongeza vifaa tiba katika zahanati, vituo vya afya pamoja na hospitali lengo ikiwa ni kutoa huduma nzuri ya matibabu kwa wananchi wote.

“Katika sekta ya afya katika kipindi hiki cha miaka minne kwa kweli tumeweza kupiga hatua kubwa sana kwani baaadhi ya maeneo katika Wilayah ii ya Kisarawe kulikuwa hakuna kabisa zahanati wala vituo vya afya lakini kwa sasa mambo yamebadilika kwani kumejengwa vituo vya afya vipya katika baadhi ya kata pamoja na zahanati hii yote ni kuhakikisha kwamba wananchi wetu hawapati usumbufu mkubwa katika upatikanaji wa matibabu na ndio maana serikali imetoa tayari shilingi milioni 400 kwa ajili ya kituo cha afya cha Msanga.”alisema Jafo.

Kwa upande wao baadhi ya wakinamama wa kata ya Msanga wamesema kwamba kukamilika kwa ujenzi wa kituo cha afya kuwaweza kuwapunguzia kero na changamoto mbali mbali ambazo wamekuwa wakikutana nazo hasa pindi wanapokenda kujifungua kwani wanatumia usafiri wa baiskeli na bodaboda kwenda kupatiwa ,matibabu kwingine kitu ambacho ni hatari kwa usalama wa maisha yao na kutoa pongeza za dhati wa serikali ya awamu ya tano katika kuboresha sekta ya afya.

Walisema kwamba katika kata ya Msanga kumekuwepo na changamoto kubwa katika suala zima la upatikanaji wa huduma ya afya hasa kwa wakinaamama japo kuwa na zahanati hivyo wana imani pindi ujenzi huo utakapokamilika utasaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa ile changamoto ya kujifunguliwa njiani.

“Kituo hiki cha afya pindi kitakapokamilika kwa upande wetu sisi kama wananchi wa kata hii ya msanga hususan kwa upande wa wakinamama tumekuwa tukipata usumbufu mkubwa sana wa kwenda umbari mrefu kwa ajili ya kutafuta huduma ya matibabu katika maeneo mengine ikiwemo kituo cha afya Manelumango hivyo baada ya miezi mitatu hali hii kwetu itakuwa ni historia kwa hiyo tunamshukuru sana Mbunge wetu Jafo pamoja na Rais we Dk John Pombe Magufuli kwa kutoa shilingi milioni 400 za ujenzi ,”walisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Musa Gama ameahidi kulitekeleza na kulisimamia agizo hilo la mradi wa ujenzi wa kituo cha afya lengo ikiwa ni kuwaondolea wanachi changamoto ya kutembea umbari mrefu kwa ajili ya kwenda kupatiwa matibabu katika maeneo mengine na kumpongeza Rais wa awamu ya tabo Dk. John Pombe Magufuli kwa kuwapatia fedha hizo.

“Kwa kweli tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa Rais wetu Dk. John Pombe Magufuli pamoja na Mbunge wetu Seleman Jafo ambaye ni Waziri wa Tamisemi kwa kuona umuhimu wa kutupatia fedha hizi kiasi cha shilingi miliono 400 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya na mimi naahidi kusimamia ujenzi huu kwa hali na mali lengo ikiwa ni kuhakikisha wananchi wetu wanapata huduma ya matibabu karibu.”alisema Gama.

KUKAMILIKA kwa mradi wa ujenzi wa kituo kipya cha afya ambacho kinajengwa katika kata ya Msanga Wilayani Kisarawe Mkoa wa Pwani kitaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa wananchi kuondokana na adha ya kutembea umbari mrefu pamoja na kuondoana usumbufu mkubwa waliokuwa wakiupata wakinamama wajawazito kwa kipindi kirefu pindi wanapotaka kwenda kujifungua.
Waziri wan chi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kisarawe akizungumza na wananchi wa kata ya Msanga hawapo pichani wakati wa ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kutembelea miradi mbali mbali ya maendeleo katika Wilaya ya Kisarawe.
 Waziri wan chi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kisarawe akisalimia na baadhi ya viongozi wa Chama cha mapinduzi CCM kata ya Msanga baada ya kuwasili katika eneo hilo akiwa katika ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kuzungumza na wananchi na kukagua miradi ya maendeleo. Baadhi ya wananchi wa Kata ya Msanga wilayani Kisarawe wakimsikiliza kwa umakini Waziri Jafo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kisarawe hayupo pichani wakati akiwahutubia wananchi hao katika mkutano wa hadhara ikiwa ni moja ya ziara yake ya kikazi ya kusikiliza kero pamoja na changamoto za wananchi.Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Mussa Gama akiwa anapokea maagizo ambayo yalikuwa yanatolewa na Waziri Jafo hayupo pichani wakati wa ziara hiyo ya kukagua miradi ya maendeleo na kuzungumza na wananchi.
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kisarawe kulia akitoa maelezo kwa viongozi wa Chama cha amapinduzi CCM na baadhi ya viongozi wa halmashauri alipotembnelea mradi wa ujenzi wa kituo cha afya chole
Baadhi ya viongozi mbali mbali wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe pamoja na baadhi ya viongozi wa Chama cha mapinduzi CCM wakisikiliza maagizo ya Waziri Jafo mara baada ya kutembelea ujenzi wa zahanati ya Kwala ambayo inajengwa kwa ajili ya kuboresha huduma ya afya kwa wananchi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kisarawe kushoto Mussa Gama akiwa katika mkutano wa adhara  ambao umeitishwa na Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo kulia kwake ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Kisarawe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...