Sampuli ya virusi vya ugonjwa vilivyochukuliwa kutoka kwa mgonjwa na kuchunguzwa katika maabara na maafisa wa serikali pamoja na wale wa shirika la afya duniani WHO zimethibitisha kwamba ugonjwa huo ni ule wa Coronavirus.

Virusi hivyo ni familia kubwa ya virusi sita na kirusi hicho kipya kitaongeza idadi hiyo kufikia saba ambapo ni maarufu kwa kusababisha maambukizi miongoni mwa binadamu.

Virusi hivyo vinaweza kusababisha homa , lakini pia vinaweza kusababisha ugonjwa mbaya wa Sars ambao uliwauwa watu 774 kati ya 8,098 walioambukizwa katika mlipuko ulioanza China 2002.

Uchanganuzi wa jeni za ugonjwa huo mpya unaonyesha kuhusishwa karibu na ugonjwa wa Sars zaidi ya ugonjwa wowote wa Coronovirus.

Mamlaka ya China imeripoti visa 139 vipya vya ugonjwa huo usiojulikana katika siku mbili, ikiwa ni mara ya kwanza kwa maambukizi hayo kuthibitishwa nchini humo nje ya mji wa Wuhan.

Visa vipya vilibainika katika miji ya Wuhan, Beijing na Shenzhen.

Korea Kusini pia iliripoti kisa chake cha kwanza kilichothibitishwa siku ya Jumatatu baada ya Thaialnd na Japan. Jumla ya visa vilivyoripotiwa sasa vinapita 200 na watu watatu tayari wamefariki kutokana na virusi hivyo.

Maafisa wa Afya wamegundua ugonjwa huo, ambao kwa mara ya kwanza ulipatikana mjini Wuhan mwezi Disemba. Wanasema umesababisha mlipuko wa homa ya mapafu lakini mengi kuuhusu haujulikani.

Wataalama nchini Uingereza waliambia BBC kwamba idadi ya watu walioambukizwa huenda ikawa kubwa zaidi ikilinganishwa na idadi iliotolewa na maafisa huku takwimu zikisema huenda imefikia watu 1,700.

China imeahidi kuongeza juhudi zake za kuchunguza wiki hii ya sherehe za kuadhimisha mwezi mpya ambapo mamilioni ya Wachina watasafiri kujiunga na familia zao.
 
KUSOMA ZAIDI BOFYA BBCswahili.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...