Waandikishaji  wasaidizi Daftari la kudumu la wapiga kura na Bvr kit Operator wametakiwa kuzingatia muda wa kufungua na kufunga ili wananchi washiriki kikamilifu katika uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.

Hayo yamesemwa na Afisa Msaidizi Mwandikishaji 
Daftari la kudumu la wapiga kura Jimbo la Tandahimba Ahmada Suleiman wakati akifungua mafunzo ya Waandikishaji wasaidizi Daftari la kudumu la wapiga kura na BVR  kit Operator

"Hakikisheni mnafungua vituo  kwa muda muafaka,siyo mwananchi anakuja wewe haupo kituoni Hapo hautaeleweka  na hautatufaa,"alisema Suleiman

Naye mwezeshaji Joseph Mongi aliwataka wanasemina hao kutunza  Bvr kit hizo kwani serikali imenunua kwa gharama hivyo zinatakiwa zitunzwe ili ziweze kwenda kutumika na maeneo mengine.
 Afisa Msaidizi Mwandikishaji  Daftari la kudumu la wapiga kura Jimbo la Tandahimba Ahmada Suleiman akifungua mafunzo kwa Waandikishaji wasaidizi na Bvr kit operator.
 Mwezeshaji Joseph Mongi akiwaelekeza Bvr kit Operator jinsi ya kutumia mashine hizo
 Bvr kit operator wakifanya mazoezi kwa vitendo
 Waandikishaji wasaidizi Daftari la kudumu la wapiga kurawakipewa mafunzo  ya uboreshaji  wa daftari la kudumu la wapiga kura

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...