Na Abdullatif Yunus wa Michuzi TV.

Katika kuendelea kutatua migogoro ya Ardhi hapa Nchini, Mkuu wa Mkoa Kagera amewaapisha Wajumbe wawili wa mabaraza ya ardhi kutoka Wilaya za Missenyi na Bukoba ili waweze kuendelea kutoa katika masuala yahusuyo katika maeneo yao.

Wajumbe hao walioapishwa Januari 20, 2020 ni Pamoja na Bi. Mary Kokuleba Mtaajwa na Bi. Jinesta Banyenza Rugakingira, katika hafla iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa Kagera, ikihudhuriwa na wadau wa sheria, Kamati ya Ulinzi na Usalama, Viongozi wa Dini, Jaji Mfawidhi wa Mahakama ya Kanda ya Bukoba, Jaji Lucia Kalio, pamoja na Jaji wa Mahakama Kuu  Kanda ya Bukoba Jaji Angela Anthony Bahati.

Wakitoa nasaha zao kwa nyakati tofauti Mara baada ya kuapishwa Kwa wajumbe hao, Viongozi hao wamewataka Wajumbe hao kusimamia na kutenda haki katika masuala yote yahusuyo ardhi hasa kutatua migogoro isiyo ya lazima, hii ni kutokana na ardhi kuendelea kuwa na Thamani kubwa katika maisha ya kila siku, na ni vyema kuendelea kuheshimu taratibu na sheria za ardhi zinvyoelekeza.
 Pichani ni picha ya Pamoja ya Wajumbe wawili walioapishwa, Viongozi wa Dini, Majaji pamoja na Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti.
Pichani ni Wajumbe wa Mabaraza ya Ardhi wakiendelea kusikiliza nasaha mbalimbali, kutoka kwa Viongozi, kutoka Kulia ni Bi. Mary Kokuleba Mtaajwa, na Bi. Jinesta Rugakingira wakati wa kuapishwa kwao.
 Pichani Ni Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa Kagera, wakifuatilia kwa Karibu matukio ya Ukumbini wakati wa hafla ya kuwapisha Wajumbe wa Mabaraza ya Ardhi.
 Pichani Ni Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba, Jaji Angela Bahati akitoa Salaam zake kwa wadau wa sheria na Wajumbe walioapishwa (hawapo pichani)
 Pichani ni Viongozi wa Dini na wadau wa sheria wakiendelea kufuatilia Kiapo cha Wajumbe wa Mabaraza ya Ardhi katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa Kagera.
 Pichani Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brig. Jen. Marco Gaguti  akisaini Miongoni mwa Hati za Kiapo cha Wajumbe wa Mabaraza ya Ardhi, wakati wa kuwaapisha Wajumbe hao.
 Pichani ni Bi. Jinesta Banyenza Rugakingira Mjumbe wa Baraza la Ardhi kutoka (W) Missenyi, akisaini hati ya Kiapo mara baada kuapishwa na Mkuu wa Mkoa Kagera.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...