Mkurugenzi Chuo cha MS TCDC Ezra Mbogori katikati akiwa anazungumza na waandishi wa habari kuhusu ya maandalizi ya Tamasha la utamaduni na sanaa (Kan investival) linalolenga kuwakutanisha watu mbalimbali likiwa na lengo la kubadilishana uzoefu pamoja na kujifunza maswala mbalimbali yahusuyo maendeleo kwa faida ya nchi yetu.


Na woinde shizza,Arusha

Wananchi pamoja na wanafunzi , vijana kutoka ndani na nje ya nchi wametakiwa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika tamasha la sanaa na utamaduni litakalofanyika januari 22 Hadi 25 mwaka huu katika chuo cha MS --TCDC mkoani Arusha.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha,Mkurugenzi wa tamasha hilo,Dave Ojay amesema kuwa,tamasha hilo linalenga kuwakutanisha watu mbalimbali likiwa na lengo kubadilishana uzoefu pamoja na kujifunza maswala mbalimbali yahusiyo maendeleo kwa faida ya nchi yetu.

Ojay amesema kuwa,uwepo wa tamasha hilo utaleta mshikamano na umoja sambamba na kujitambua hasa katika maswala ya maendeleo ambapo litawalenga watu mbalimbali hususani Vijana wa vyuo vya elimu ya juu .

Amesema kuwa,katika tamasha hilo watawashirikisha waoneshaji mbalimbali wa Sanaa na tamaduni ambao wataweza kuwakilisha ujumbe wao kupitia Sanaa,tamaduni na muziki lengo likiwa ni kubadilishana mawazo na kuendeleza mahusiano.

Mkurugenzi Mkuu wa chuo hicho,Ezra Mbogori amesema kuwa,uwepo wa tamasha hilo utasaidia Sana kubadilishana mawazo baina ya wanafunzi hao wa vyuo na wageni kutoka nchi mbalimbali .

"Kiingilio katika tamasha hilo ni 15,000 kwa watu wazima na 5,000 kwa watoto huku watoto wenye umri chini ya miaka 12 wataingia bure ,hivyo nawaomba Sana mjitokeze kwa wingi katika tamasha hili kwani lina fursa za kutosha."amesema.

Naye Mkurugenzi wa mipango wa chuo hicho, Sara Teri alitaja wanamuziki watakaoshiriki katika tamasha hilo kuwa Ni mwanamuziki kutoka nchini Tanzania ,Fid Q,Vitali Maembe ,Sandra Nankoma kutoka Uganda ,Juma Tutu kutoka Kenya ,Victor Kunonga kutoka Zimbabwe,Isabella Novela kutoka Mozambique .

Ametaja nchini zitakazoshiriki tamasha hilo kuwa ni pamoja na Kenya,Tanzania,Uganda, Mozambique,Burundi, Zimbabwe,Afrika Kusini na Congo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...