Meneja uendeshaji wa Kiwanda cha
kuzalisha tofali cha SHAFA Bw. Suleiman Amour akimuonesha Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki matofali
yanatengenezwa na kiwanda hicho wakati wa ziara yake ya kikazi tarehe 20
Januari, 2020 Wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akiwa katika ziara yake ya kikazi
katika kiwanda cha kutengeneza matofali cha SHAFA kilichopo Wilaya ya
Mkuranga Pwani.
Meneja uendeshaji wa Kiwanda cha
kuzalisha tofali cha SHAFA Bw. Syleiman Amour akimuonesha Waziri wa Nchi
Ofiis ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki namna matofali
yanavyotengenezwa katika kiwanda hicho.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akioneshwa mtaambo maalum wa
kutengeneza matofali na Meneja uendeshaji wa Kiwanda cha kuzalisha
tofali cha SHAFA Bw. Suleiman Amour wakati wa ziara yake kiwandani hapo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akiuliza jambo kuhusu namna
matofali yanavyosafirishwa katika kiwanda cha kutengeneza tofali cha
SHAFA kwa Meneja uendeshaji wa Kiwanda cha kuzalisha tofali cha SHAFA
Bw. Suleiman Amour akimuonesha
Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akizungumza na
watumishi wa kiwanda cha kutengeneza tofali cha SHAFA (hawapo pichani)
wakati wa ziara yake kiwandani hapo.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
……………
MWANDISHI WETU
Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji Mhe. Angellah
Kairuki ametembelea na kukagua mazingira ya uendeshaji wa kiwanda cha
vifaa vya ujenzi cha SHAFA na kupongeza uzalishaji wa tofali kiwandani
hapo na kusema ni wa kuridhisha.
Ametoa pongezi
hizo alipotembelea kiwandani Januari 20, 2020 ikiwa ni sehemu ya ziara
yake ya kikazi katika Mkoa wa Pwani ili kukagua mazingira ya wawekezaji,
kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili ili kuendelea kuwa na
mazingira mazuri ya wafanya biashara na wawekezaji nchini.
Aidha katika
ziara yake aliambatana na Watendaji kutoa Ofisi yake, Uongozi wa Mkoa wa
Pwani, Watendaji kutoka Wilaya ya Mkuranga pamoja na watendaji wa
Taasisi za Serikali ikiwemo TANESCO, TARURA, TRA, na Kituo cha Uwekezaji
nchini (TIC).
Akizungumza na
waandishi wa habari kiwandani hapo, alisema amevutiwa na uwekezaji
katika kiwanda hicho kwa kuwa na matofali bora kwa kuzingatia muhimu wa
mahitaji ya ujenzi katika kuhakikisha kuna kuwa na majengo bora, kiasa
na imara kwa matumizi mbalimbali.
“Vipo viwanda
zaidi ya vitatu vinavyotengeneza tofali nchini ingawa hiki kinaongoza
kwa kuwa na mitambo ya kisasa aina ya MASA yenye uwezo wa kuzalisha
tofali 10,000, vigae vya sakafuni zaidi ya 10,000 kwa siku
ukilinganisha na viwanda vingine na kwa nchi za Afrika Mashariki ni
kiwanda cha mfano kwa kutoa matofali yenye ubora wa hali ya
juu,”alesisitiza Waziri Kairuki.
Alieleza kuwa,
ipo haja ya kuunga mkono jitihada za wawekezaji wa viwanda kama hivyo
ili kuendelea kujieletea maendeleo ya nchi kwa ujumla kwa kuzingatia
mchango wake katika ngazi zote kuanzia Kijiji, Taifa hadi nje ya nchi.
Aliongezea kuwa ,
furaha yake ni kuona kiwanda kinaweza kuzalisha kwa haraka, ubora na
idadi kubwa kwa siku ili kuhakikisha kuna kuwa na majengo salama na
yenye kudumu hadi vizazi vijavyo.
Akiwasilisha
taarifa ya kiwanda kwa waziri, Afisa Mahusiano wa kiwanda hicho Bw.
Agrey Roodluck alieleza malengo ya mradi ni pamoja na kuongeza wigo
katika sekta ya ujenzi kwa kuzingatia uzalishaji wake unalenga kuwa na
aina tofauti tofauti za matofali yenye ubora na kuweza kukidhi mahitaji
kwa gharama nafuu.
“Mradi
umezingatia changamoto zilizopo za ukosefu wa matofali bora katika
maeneo mengi yanayohitajika katika ujenzi wa maegesho ya magari,
bararaba, maeneo ya viwanja vya ndege pamoja na majengo makubwa na
madogo,”alieleza Roodlucky
Aidha alitoa omba
kwa waziri kuendelea kuhamasisha ujenzi salama wa majengo ya taasisi,
nyumba ndogo na kubwa kwa kuendelea kutumia tofali za kiwanda hicho na
kueleza kuwa ni sehemu ya kuunga mkono maendeleo ya nchi kwa kuzingatia
malighafi zinazotumika zinatoka nchini.
“Hadi kukamilika
kwa mradi huu utatumia jumla ya Tshs Bilioni 15.3 na tayari zaidi ya
asilimia 90 zimeshatumika na asilimia 99.9 za malighafi za kiwanda
zinatoka hapa hapa nchini ikiwemo saruji, mchanga, kokoto na
maji,”alisisitiza
Sambamba na hilo
alisema, lengo kuhakikisha kiwanda kinatoa mchango katika pato la taifa
katika kuhakikisha kinalipa kodi zote zinazotakiwa na kuendelea
kuzalisha ajira zaidi ya 100 zitakazozingatia kundi kubwa la vijana
wazawa ili kuweza kuendesha mitambo iliyopo.
Naye Mkuu wa
Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga alimshukuru waziri kwa kutembelea
mradi huo, na kueleza kuwa, ni mradi wenye faidi katika Wilaya yake kwa
kuzingatia mchango wa mradi na namna walivyojikita katika kuhakikisha
wanakuwa wenye bidhaa bora na kukidhi mahitaji ya wateja wake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...