Na Mwandishi wetu Globu ya jamii
KUFUATIA Mchezaji wa Timu ya Taifa Mbwana Sammatta kujiunga na timu ya soka ya Aston Villa, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Mb) amempongeza nahodha na mchezaji wa Timu ya Tanzania (Taifa Stars) kwa kufanikiwa kujiunga na timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu nchini Uingereza (EPL) na kuwa Mtanzania wa kwanza kuchezea Ligi Kuu nchini humo.

hayo yameelezwa kwenye taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Eleuteri Mangi jijini Dar es Salaam leo, huku ligi hiyo ikiendelea kuchezwa nchini Uingereza.

"Serikali na Watanzania wote tunajivunia mafanikio ya kijana wetu Samatta katika soka, kuingia kwake kwenye ligi kuu nchini Uingereza kumefungua milango kwa vijana wengi wa Kitanzania kwenda kucheza soka  kulipwa katika nchi mbalimbali duniani, hakika ameonyesha uzalendo mkubwa kwa nchi yetu". Amesema Dkt. Mwakyembe.

Hata hivyo Samatta Kabla ya kujiunga na klabu ya Aston Villa alikuwa akichezea klabu ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji na aliiwezesha klabu hiyo kushinda taji la ligi ya Ubelgiji mwaka 2019 pamoja na kufuzu michuano ya Ulaya.

Mbwana Samatta alimaliza msimu huo akiwa mfungaji bora wa ligi ya Ubelgiji na akashinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa ligi ya Ubelgiji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...