Na Jumbe Ismailly DODOMA

WIZARA ya Mifugo na Uvuvi imesambaza jumla ya lita 1,281.5 za dawa za kuogeshea mifugo kwa mikoa ya Dodoma na Singida katika zoezi la awamu ya kwanza la kampeni za uogeshaji mifugo lililofanyika katika mikoa hiyo

Aidha daktari huyo wa mifugo amefafanua kwamba mazoezi ya kuogesha mifugo katika nchi nzima yalikuwa yamepata changamoto kwa hali hiyo yaliacha kufanyakazi,lakini baada ya kutafuta changamoto zilizosababisha hayo,ikagundulika badhi ya changamoto ikiwemo gharama za ununuzi wa dawa za kuogeshea mifugo na ubovu wa majosho.

Hata hivyo msemaji huyo wa wizara amesisitiza kuwa kutokana na ubovu huo wa majosho wizara imeanza kuyafanyia ukarabati majosho ili kuondokana na changamoto zilizokuwepo za kukosa dawa na ubovu wa majosho ziweze kuondoka na zoezi la uogeshaji mifugo liweze kuendelea kama lengo la serikali linavyotaka.

Akizungumzia kuhusu zoezi la uogeshaji kwa kanda ya kati,Dkt. Mngumi ameweka bayana kwamba,kiwango cha awali cha uogeshaji kwa mwezi kilikuwa jumla ya mifugo 186,000 na kwamba katika kipindi cha kuanzia mwezi Nov,mwaka jana hadi sasa jumla ya michovyo 188,000 imeogeshwa kwenye majosho yanayofanyakazi.

Kwa upande wao baadhi ya wafugaji waliopeleka mifugo yao kuogesha wameiomba wizara ya mifugo na uvuvi kuendelea kuwapatia dawa ya ruzuku kwani kuwepo dawa hizo kutawasaida wafugaji kupata hamasa ya kupeleka mifugo yao kuogesha maana kuna wakati hushindwa kupeleka mifuo yao kutokana na kukabiliwa na hali ngumu ya uchumu.

Naye daktari wa mifugo wa Jiji la Dodoma,Innocent Peter ameweka bayana kwamba ng’ombe wanaokufa kwa ugonjwa wa homa ya mapafu,vifo hivyo havisababishwi na kutoogeshwa kwa sababu ugonjwa huo hausababishwi na kupe.
Mkazi wa Kijiji cha Mkoyo,Kata ya Hombolo,Mkoani Dodoma akijaribu kuokoa maisha ya mbuzi wake aliyenusurika kunywa maji yenye dawa ya kuogeshea mifugo wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya kuogesha mifugo Kanda ya kati uliofanyika Kijiji cha Mkoyo.(Picha zote Na Jumbe Ismailly)
Baadhi ya mifugo ya wafugaji wa Kijiji cha Mkoyo,Kata ya Hombolo,Mkoani Dodoma wakisubiri kuingizwa kwenye josho la kuogeshea mifugo ili waweze kuoga kwa lengo la kupunguza na kama siyo kumaliza kabisa magonjwa yatokanayo na kupe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...