RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo Febuari 3, 2020 amewaapisha viongozi wateule viongozi mbalimbali aliowateua Januari 31,2020  Ikulu  jijini Dar es Salaam.

Viongozi waliowateua ni Makatibu wakuu,Naibu katibu Mkuu, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Kamishna wa Ardhi, Makamishina wa Tume ya utumishi wa Mahakama na Msajili wa Mahakama.

Makatibu wakuu ni  Mary Makondo, kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Kabla ya uteuzi huo Mary Gasper Makondo alikuwa Kamishna wa Ardhi katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Anachukua nafasi ya Doroth Mwanyika ambaye amestaafu.

Dkt. Hassan Abbas kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Kabla ya uteuzi huo Dkt. Hassan Abbas alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo. Anachukua nafasi ya Suzan Mlawi ambaye amestaafu.

Prof. Riziki Silas Shemdoe kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara. Kabla ya uteuzi huo Prof. Riziki Silas Shemdoe alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma. Anachukua nafasi ya Prof. Joseph Buchweishaija ambaye amestaafu.

Zena Ahmed Said kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati. Kabla ya uteuzi huo alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Tanga. Anachukua nafasi ya Dkt. Hamis Mwinyimvua ambaye amestaafu.

Christopher Kadio kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kabla ya uteuzi huo alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza. Anachukua nafasi ya Meja. Jen Jacob Kingu ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.

Rais Dkt. Magufuli amemuapisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Leonard R. Masanja, Kabla ya uteuzi huo alikuwa Kamishna wa Umeme na Nishati Mbadala.

Kwa Upande wa Makatibu wakuu tawala za mikoa, Rais amewaapisha Makatibu wakuu watatu ambao ni Judica Haikase Omari kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Stephen Mashauri kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma na Emmanuel Mpawe Turuba kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza.

Wakuu wa vyomo vya ulinzi na Usalama Rais Dkt. Magufuli amewaapisha Brig. Jen. Suleiman Mungiya Mzee kuwa Kamishna Jenerali wa Magereza. Brig. Jen. Suleiman Mungiya Mzee anachukua nafasi ya Phaustine Kasike ambaye ameteuliwa kuwa Balozi,Naibu Kamishna wa Magereza DCP John William Hasunga kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. DCP John William Hasunga anachukua nafasi ya Thobias Andengenye ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Hata hivyo kamishina wa Ardhi, amemwapisha Nathaniel Mathew Nhonge kuwa Kamishna wa Ardhi katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Kabla ya uteuzi huo Nathaniel Mathew Nhonge alikuwa Kamishna wa Ardhi Msaidizi Kanda ya Dar es Salaam na Pwani.

Kwa Upande wa Wasajili wa mahakama Rais Dkt. Magufuli amewaapisha Wilbert Chuma kuwa Msajili Mkuu wa Mahakama,Kelvin Mhina kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani na Shamira Sarwat kuwa Msajili wa Mahakama Kuu.

Makamishna wa Tume ya utumishi wa mahakama amewaapisha Jaji Dkt. Gerels Ndika kuwa Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama, wakili  Julius Kalolo Bundala kuwa Makamishna wa Tume ya Utumishi wa mahakama na wakili  Genoveve Kato kuwa Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...