Na Mwandishi Wetu,Michuzi Globu ya jamii

KITUO  cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) wanaratibu ziara ya wawekezaji na wafanyabiashara wa Tanzania kwenda nchini Indonesia, Singapore na Thailand kwa lengo la kutafuta fursa za ushirikiano katika uwekezaji na biashara kupitia maeneo ya ubia, masoko na teknolojia.  Kiongozi wa msafara atakuwa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki.

 Taarifa iliyotolewa na TIC kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam imesema kuwa katika ziara hiyo kutafanyika kongamano la siku moja kila nchi kati ya Tanzania na nchi husika (Indonesia, Thailand na Singapore) ili kuwakutanisha ana kwa ana wafanyabiashara/wawekezaji wa Tanzania na nchi hizo.

Ambapo watatumia nafasi hiyo kujadiliana uwepo wa fursa mbalimbali za kibiashara na uwekezaji zinazoweza kuanzishwa na kuendelezwa katika sekta mbalimbali. Sekta lengwa ni viwanda, kilimo, ujenzi, mawasiliano, madawa na vifaa tiba, madini, fedha, utalii, TEHAMA na biashara kwa ujumla.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ni kwamba ujumbe huo utaondoka nchini Februari 23 mwaka huu wa  2020 na kushiriki  makongamano kama ifutavyo; Kongamano kati ya Tanzania na Indonesia ni tarehe 24 Februari 2020, Kongamano kati ya Tanzania na Thailand ni tarehe 26 Februari, 2020 na Kongamano kati ya Tanzania na Singapore ni tarehe 28 Februari, 2020.

 TIC imesema kila mshiriki atajigharamia usafiri, malazi na chakula kwamba wanawakaribisha wadau wenye nia ya kushiriki katika ziara hiyo wajisajili kupitia TPSF kwa barua pepe events@tpsftz.org au simu +255 682 031 728/ +255 0784 323068. 

Na kwa mawasiliano zaidi; tembelea ofisi za TIC Makao Makuu zilizopo Dar es Salaam mtaa wa Shaaaban Robert, jirani na ofisi ndogo za Bunge au wasiliana na Benson Nkini kwa namba 0715923777 au Diana Ladislaus kwa namba 0719653079.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...