Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam  Paul Makonda amesema ametangaza vita  kuwashughukikia kikamilifu wanaume wenye tabia ya kuwaonea Wanawake kwa kuwapiga hadi kuwaharibu mwonekano wa sura,macho,kuwavunja meno au taya na kusababisha baadhi yao kupata ulemavu wa kudumu jambo ambalo ni kinyume na Sheria.

Makonda ameyasema hayo wakati wa maadhinisho ya siku ya Wanawake Duniani kwa Mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika katika viwanja vya Leaders .

RC Makonda amesema Mwanamke yeyote atakaeshushiwa kipigo na Mwanaume kuanzia sasa atoe taarifa kupitia simu ya mkononi namba 0682009009 ili mwanaume alietenda ukatili huo atafutwe popote alipo na kuchukuliwa hatua Kali za kisheria.

Aidha RC Makonda amesema baadhi ya Wanaume wamekuwa na tabia ya kuwadharau wanawake kutokana kutokuwa na elimu au kipato jambo ambalo amesema hawezi kulivumilia katika mkoa huo.

Katika hatua nyingine RC Makonda amesema amepanga kuliomba Bunge linapofanya Mabadiliko ya Sheria ya ndoa kiongezwe kipengele cha kutaka 40% ya Mshahara wa Mwanaume apatiwe mwanamke asiefanya kazi kwaajili ya Shughuli za familia ili kumjengea uwezo Mwanamke.*

Pamoja na hayo RC Makonda amewataka Wanawake kutojisahau katika suala zima la malezi ili kuwaepusha watoto na makundi mabaya ikiwemo Matumizi ya Dawa za kulevya, Ushoga, Usagaji,  Wizi na Uporaji.

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza katika maadhinisho y siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.
 Wafanyakazi Wanawake  wa Madini wakiongozwa na Shirika la Madini wakiwa Katika maandamo ya Maadhinisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.
 Wafanyakazi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) wakiwa katika maandamo ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.
 Wafanyakazi Wanawake wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) wakiwa Katika maandamo ya Maadhinisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika katika vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Sarah Msafiri akitoa maelezo namna walivyoratibu maadhinisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.
 Wafanyakazi Wanawake wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wakiwa Katika maandamo ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.
 Wafanyakazi  Wanawake wa Bodi  ya mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) wakiwa katika maandamo ya Siku ya Maadhinisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...