Vikundi vya wachimbaji wadogo Wilayani Kishapu wakifanya maandalizi ya kuchenjua mchanga wa almasi katika eneo lilioko nje kidogo ya mji mdogo wa Maganzo Shinyanga.
Vikundi vya wachimbaji wadogo Wilayani Kishapu wakifanya maandalizi ya kuchenjua mchanga wa almasi katika eneo lilioko nje kidogo ya mji mdogo wa Maganzo Shinyanga.
Sophia Kasenga Msimamizi wa Kikundi cha Oyster bay Family akionesha punje ya almasi iliyopatikana baada ya kikundi chake kuchuja mchanga wa almasi jana nje kidogo ya mji mdogo wa Maganzo Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyamaganga Talaba akikagua mchanga wa almasi kujionea mapungufu yaliyopo katika zoezi la uchenjuaji wa mchanga wa almasi kwa vikundi vya wachimbaji wadogo wadogo wa madini nje Kidogo ya mji mdogo wa Maganzo ulioko Wilayani Kishapu Shinyanga. 

Na mwandishi wetu Shinyanga
VIKUNDI vya Wachimbaji wadogo wa madini ya almasi, wilayani Kishapu, mkoani Shinyanga, wameanza kunufaika na marudio ya mchanga wa almasi kutoka mgodi Williamson Diamond limited, kufuatia agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli kuwaruhusu wachimbaji hao kunufaika na madini hayo huku tahadhari ya ugonjwa corona ikiwa imechukulia.

Wachimbaji hao wadogo wakiwa katika vikundi tofauti waliendelea kuchenjua mchanga wa almasi uku wakichukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa corona na baadhi yao wakiwa wamefanikiwa kupata punje ndogo za almasi kutoka kwenye mchanga huo.

Bi.Mercy Shirima Msimamizi wa Kikundi cha Masenga Miners akiongea na vyombo vya habari alisema kikundi chake kimeweza kupata vipande vitatu vidogo vya almasi na kuwataka wachimbaji hao kuendelea na kazi hiyo kwa moyo ili kuweza kufiki lengo la kunufaika na madini hayo.

Akiongea na wachimbaji hao Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Bi. Nyabaganga Taraba amewataka wachimbaji hao kuwa makini na taadhari ya ugonjwa wa mlipuko wa Corona kwa kuhakikisha wanaepuka msongamano na kumtaka kila mmoja kuwa sabuni na kunawa mikono kila wakati.

Siku ya kwanza ya zoezi ilo imekuwa na changamoto ya kukatika kwa maji lakini pia baadhi ya wachimbaji walidai mchanga unaoletwa katika eneo hilo kutoka mgodi wa Mwadui haufai na badala yake wangeshirikiwa kuchagua mchanga wa kuchenjua kwani wana uzoefu na mchanga huo.

‘’Watuchukue sisi wazoefu wa kazi kwa sababu sio raisi kwa muda wote huu kuchuja mchanga na usipate chochote na huu ni ushauri wangu kwa viongozi wakitutumia sisi wazoefu kuchagua mchanga zoezi ili litakua na mafanikio makubwa.’’ Alinukuliwa akisema Bw.Jayunga James Mchimbaji mdogo. 

Wachimbaji hao wadogo wa madini ya almasi katika mji mdogo wa Maganzo wilayani kishapu wameanza rasmi kunufaika na madini hayo,huku wakiipongeza serikali kwa kuwajali wananchi wa shinyanga hasa wachimbaji wadogo wa madini hayo.

Serikali tayari imefanya marekeabisho ya sheria ya madini na kupiga marufuku usafirishaji wa makinikia nje ya Nchi na zoezi hili tayari limeanza kuwanufaisha wananchi ambao baadhi yao kwa zioezi hili tayari wamepata madini ambayo yatasaidia kuwainua kiuchumi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...