Akiongea mara
baada ya kumalizika kwa mkutano huo, Mwenyekiti wa mkutano ambae ni Katibu Mkuu
Wizara ya Mambo ya Nje na UShirikiano wa Afrika Mashariki, Brigedia Jenerali,
Balozi Wilbert Ibuge amesema kuwa lengo la mkutano huo lilikuwa ni kuangalia
mambo mawili makubwa ambayo ni dhima ya SADC kuanzia sasa 2020 hadi 2050 pamoja
na mpango mkakati wa SADC kuanzia mwaka 2020 - 2030 kwa sababu mpango mkakati
wa SADC uliokuwa unatumika tangu mwaka 1992 umeisha muda wake.
"Nyaraka
hizi mbili ni za muhimu sana kwa sababu hadi sasa hivi toka SADC ilipoanzishwa
1992 imefanya mambo makubwa lakini sasa ule mpango mkakati wake uliokuwa
unatumika tangu mwaka 2010 na ambao ulihuishwa mwaka 2015 ukafika hadi 2020 umeisha
muda wake hivyo ilikuwa ni muhimu kuandaa rasimu ya nyaraka hizi muhimu,"
Amesema Balozi Ibuge.
Ameongeza
kuwa, rasimu za nyaraka hizo mbili zitawasilishwa kwenye mkutano wa 40 wa Wakuu
wa nchi wanachama wa SADC na Serikali unaotegemewa kufanyika tarehe 17 Mwezi Agosti
2020 kwa njia ya mtandao.
Mpango
Mkakati wa SADC ni mpango wa maendeleo ya kanda uliopitishwa na Mkutano wa
wakuu wa nchi na serikali wa SADC uliofanyika mwaka 2003 jijini Dar es Salaam
na ulianza kutekelezwa rasmi mwaka 2005 kwa kipindi cha miaka 15 (2005 - 2020). Aidha, mpango huo una vipaombele
vinne ambavyo ni maendeleo ya viwanda na mtangamano wa soko, miundombinu bora,
amani na usalama, pamoja na programu maalum.
"Dira ya
SADC 2020 - 2050 inatoa taswira ya Jumuiya kwa miaka 30 ijayo ambapo msingi
wake ni amani, ulinzi, utulivu na utawala bora, uchumi wa kati unaoendeshwa na
sekta ya viwanda na wanajumuiya wenye hali bora ya maisha," Amesema Balozi
Ibuge.
Hivyo dira ya SADC 2050 ni muhimu kwa maendeleo ya Ukanda wa Kusini mwa Afrika hususan katika kutekeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Dunia 2030 na ajenda ya Umoja wa Afrika ya Mwaka 2063.
Katika tukio
jingine, Brigedia Jenerali, Balozi Wilbert Ibuge amekutana na kufanya amekutana
na kufanya mazungumzo na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia
Wakimbizi Duniani (UNHCR) nchini Tanzania, Bw. Antonio Canhandula katika ofisi
ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Balozi
Wilbert Ibuge amesema kuwa UNHCR imekuwa na mchango mkubwa sana unaohusisha kulinda
haki za wakimbizi lakini pia kuwarejesha wakimbizi nchini mwao.
Pamoja na mambo mengine, mazungumzo yalilenga kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) kwa ujumla.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) nchini Tanzania, Bw. Antonio Canhandula akiongea na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na UShirikiano wa Afrika Mashariki,Brigedia Jenerali, Balozi Wilbert Ibuge katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na UShirikiano wa Afrika Mashariki, Brigedia Jenerali, Balozi Wilbert Ibuge pamoja na baadi ya maafisa waandamizi wakifuatilia mkutano.Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na UShirikiano wa Afrika Mashariki, Brigedia Jenerali, Balozi Wilbert Ibuge akimuelezea jambo Mwakilishi UNHCR nchini Tanzania, Bw. Antonio Canhandula
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...