Na Said Mwishehe,Michuzi TV

VYAMA vya siasa nchini vimetakiwa kufanya kampeni za kistaarabu na kuepuka kufanya fujo au kuchochea vurugu ya aina yoyote katika mikutano ya vyama vingine ,kutotumia lugha ya matusi ,kashfa,kejeli, udhalilishaji na vitisho au kugha inayochochea uvunjifu wa amani  au ubaguzi wa kijinsia ,ulemavu,rangi au maumbile kwenye shughuli za kampeni wa Uchaguzi Mkuu mwaka huu.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) Jaji mstaafu Semistocles Kaijage amesema hayo leo Agosti 1,2020 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na vyama vya siasa kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka hu ambapo ameeleza pia ni vema wagombea na wafuasi wao kutobeba silaha yeyote ikiwa pamoja na silaha za jadi au zana yoyote inayoweza kumdhuru mtu katika mikutano na shughuli zote za kampeni au mkusanyiko wowote wa kisiasa.

"Nawasihi kusoma na kuzingatia ipasavyo kanuni za maadili ya uchaguzi ili kuepuka usmbufu unaoweza  kuwapata na kuathiri haki yenu ya kufanya kampeni kwa ajili ya kunadi wagombea wenu  na kuelezea sera zenu.

"Pamoja  na kueleza na kunadi sera na Ilani za vyama vyenu,kipindi cha kampeni kitumike pia kuwamasisha wananchi hasa wapiga kura waliojiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura,"amesema.

Aidha maadili hayo yanahusisha  pia mamlak ya uundaji wa kamati za maadili kuanzia ngazi ya kata,jimbo taifa na rufaa.Hivyo amewashauri wazitumie kamati hizo kipindi cha kampeni  pale kunapokuwa na malalamiko kwani zimepewa uwezo wa kisheria wa kushughulikia malalamiko kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa na wajumbe wake ni pamoja na wawakilishi wa vyama vya vitakavyoshiri uchaguzi katika ngazi husika.

Wakati huo huo Jaji Mstaafu Kaijage amesema kumekuwepo na malalamiko kwa baadhi ya watendaji wa uchaguzi kutokuwepo ofisini wakati wa uteuzi wa wagombea .Kitendo cha aina hiyo ni kinyume cha maadili ya uchaguzi zinawataka watendaji wa uchaguzi kuwa katika maeneo yao ya kazi muda wote wakati wa kipindi cha uteuzi wa wagombea ,upigaji kura na katika hatua yoyote ya mchakato wa uchaguzi.

"Tume tayari imekutana na wasimamizi wote wa uchaguzi kwa upande wa Tanzania Bara Julai 24 mwaka huu jijini Dodom ambapo msisitizo uliotolewa kwa wao kuzingatia maadili ya uchaguzi na maelekezo yanayotolewa ,aidha wasimamizi wa uchaguzi tayari wamekwisha kuteuliwa na wanaendela na mafunzo ambayo yatakamilika Agosti 3,2020,"amesema.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) Jaji mstaafu Semistocles Kaijage.PICHA NA MICHUZI JR-MMG.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...