MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.John Magufuli


Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Kigoma 


MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.John Magufuli amesema kuwa kiasi cha Sh.bilioni 799.52 zimetumika miradi ya kimkakati ya kuendeleza miji nane katika mikoa mbalimbali nchini ambapo kwa Mji wa Kigoma ulitengewa Sh

.bilioni 31.19. 


Akizungumza leo Septemba 18, 2020 mbele ya maelfu ya wananchi wa Mkoa wa Kigoma , Dk.Magufuli ambaye yupo kwenye mikutano yake ya kuomba ridhaa ya kuchaguliwa tena katika nafasi ya urais, ameitaja miji mingine iliyopo kwenye mkakati huo ni Arusha, Manispaa ya Mtwara Mikindani, Mwanza, Manispaa ya Ilemela, Mbeya, Tanga na Dodoma. 


"Mkiona mtu anasimama mbele ya wananchi wa Kigoma halafu anasema mradi wa kuuboresha miundombinu ya Mji wa Kigoma amefanya nini maana yake hata Dododma amepeleka , msema kweli siku zote mpenzi wa Mungu , tujiepushe na matapeli wa kisiasa na kwenye siasa matapeli wapo.Nitasema ukweli , mradi wa kuendeleza hiyo miji ipo katika Ilani ya Uchaguzi Mkuu 2015 hadi 2020,"amesema Dk.Magufuli. 


Amesema kwa upande wa Kigoma kupitia mradi wa kuendeleza miji nane, imewezesha kujengwa kwa barabara ya kilometa 15.13, kujengwa mifereji pamoja na dampo la kisasa , wakati kwa Dodoma mradi huo umewezesha kujengwa soko , stendi ya kisasa, na taa za barabarani. 


"Mtu asimame alete umaarufu wake na kusema kuwa taa tumeweka hapa, bali tumeweka maeneo mengi tu , tunatekeleza miradi hii bila kubagua upinzania, kwa mfano Arusha kiongozi alikuwa Chadema lakini tumeweka mradi , Mikindani kulikuwa na CUF lakini tumeboresha, ndio dhana ya kuwa maendeleo hayana Chama,"amesema Dk.Magufuli. 


Akizungumzia zaidi kuhusu maendeleo ambayo yamefanyika Mkoa wa Kigoma Dk.Magufuli amesema katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kiasi cha Sh.bilioni 567 zimetumika kwa ajili ya miradi ya barabara. 


"Katika kipindi kifupi Kigoma haitakuwa na tatizo la barabara kutokana na fedha hizo ambazo zimetengwa ... Kigoma mkae mkao wa kutengeneza biashara baada ya barabara kukamilika,"amesema Dk.Magufuli na kuongeza "Hii ndio Tanzania ninayoitaka, ndio Kigoma ninayoitaka, huu ni wakati wa kujipanga katika miradi ya maendeleo na hivyo kutengeneza ajira" .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...