Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Bagamoyo

RAIS Mstaafu katika Serikali ya Awamu ya Nne Jakaya Kikwete amesema chini ya uongozi Rais Dk.John Magufuli nchi ameiongoza ameongoza vizuri mengi mazuri yamefanyika, hivyo wananchi wataionesha shukrani yao kwa kumchagua kwa kishindo katika Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 28 mwaka huu.

Kikwete amesema hayo leo katika mkutano wa kampeni za mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dk.Magufuli aliyefika kwa wananchi wa Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani kuwaomba ridhaa ya kuongoza nchi kwa miaka mitano mingine ili aendelee kuleta maendeleo zaidi ya yaliyofanyika miaka mitano iliyopita.

Akizungumza zaidi mbele ya maelfu ya wananchi hao na mgombea urais wa CCM, Kikwete amesema wananchi wanatambua kazi ambayo imefanywa na Rais Magufuli, hivyo hana shaka hata kidogo kuwa atashinda kwa kishindo."Wananchi wataionesha shukrani yao kwako kwa kukupa kura nyingi.

"Endelea kupambana na endelea kuamini hakuna kitakachoharibika, hapa Bagamayo wagombea ubunge wameelezea vizuri sana yale ambayo yamefanyika, nchi imepiga hatua kubwa kuliko wakati nakukabidhi nchi, na kubwa zaidi nchi imetulia".

Kikwete amempa pole na hongera Dk.Magufuli na kwamba mpaka sasa sasa amefanya kazi kubwa na nzuri, ameendesha kampeni vizuri."Sina wasiwasi utashinda, utashinda, utashinda sana na Chama chetu kitashinda, sioni hofu wala sababu ya CCM kushindwa, mgombea urais kushindwa, wabunge wengi na madiwani kushindwa.

"Nakupa pole kwa kazi kubwa unayofanya ya kampeni, nimeifanya, naijua ugumu wake, naijua adha yake, lakini naijua raha yake.Unakuwa umechoka sana lakini ukikuta wana CCM wamejaa , wanafuraha roho yako inakuwa baridi".

Wakati anaanza kuzungumza katika mkutano huo, Kikwete alimwambia Dk.Magufuli kwamba baada ya kupata taarifa kuwa leo atakuwa Bagamoyo mkoani Pwani aliona ni vema naye akawepo."Nikasema lazima niungane na wana Bagamoyo, hapa mimi ni nyumbani kabisa tena kwa kuzaliwa, hivyo nimeungana na wana Bagamoyo wenzangu na Wana Pwani kukukaribisha, kukupongeza na kukupa pole."

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...