NA MWAMVUA MWINYI,BAGAMOYO

WAKALA wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (Ruwasa) na Dawasa wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, wamedhamiria kumaliza kero ya maji kwa wakazi wilaya Bagamoyo , pamoja na Mji wa Vikawe uliopo Kibaha Mji.

Hayo yameelezwa na Kaimu Meneja wa Ruwasa wilayani humo Mhandisi James Kionaumela na Meneja wa Dawasa Judith Singirika, wakikagua miradi hiyo ya ujenzi wa vituo vya kusukumia maji, matenki ya kuhifadhia sanjali na vituo vya kuchotea katika Vijiji vya Kata za Mapinga, Kerege, Yombo, Makurunge na Fukayosi.

Kionaumela alieleza, wilaya ina vyanzo vikuu viwili ambavyo ni maji ya chini ya ardhi yanayopatikana kwa kupitia uchimbaji wa visima, na kwamba kuna visima 215 kati ya hivyo 190 vinatumia pampu ya mikono.

"Kupitia mpango wa malipo kwa matokeo ya (PbR) wilayani hapa iliyoanzishwa kwa sheria namba 5 ya mwaka 2019, imefanya upanuzi wa mradi uliopo Kitongoji cha Chombe Juu kwenda Chamgoi Kata ya Kiromo uliogharimu kiasi cha shilingi milioni 54.2," .

Aliongeza kuwa mradi mwingine upo Kitongoji cha Mtoni Kata ya Makurunge unaotekelezwa na (NWF), kwa bajeti ya mwaka wa fedha wa 2019/2020 kupitia wataalamu wa ndani ambao unagharamu kiasi cha shilingi milioni 181.4, ikitumia mafundi wa ndani.

"Sanjali na hayo pia tuna mradi mwingine katika Kitongoji cha Kuluwi kupitia mfuko huohuo wa NWF kwa bajeti ya mwaka 2019/2020, ujenzi huo unagharimu shilingi milioni 229.9, miradi yote kwa ujumla inalenga kuwaondolea adha wakazi wanaoishi katika maeneo yao", alibainusha Kionaumela.

Nae Meneja wa Dawasa wilaya Judith Singirika alimwambia Kawawa kuwa ujenzi wa tenki katika Kitongoji Kibosha Kata ya Mapinga utakwenda kumaliza kero hiyo katika maeneo ya Vikawe Kibaha Mji, Nyakahamba, Kerege, Kitonga, Kimele, Mingoi ikiwemo Kibosha yenyewe ambapo watu zaidi ya 50,000 watanufaika na huduma hiyo.

"Hapa tunajenga kituo tutachofunga pampu itayosukuma maji kutoka chanzo cha Ruvu chini, pale Vikawe kuna ujenzi wa tenki kubwa linalolenga kuboresha upatikanaji wa maji kwa wananchi wetu katika maeneo tofauti yakiwemo ya Kitongoji cha Nyakahamba kinachokabiliwa na adha hii," alisema Mhandisi Singirika.

Kawawa alisema , Rais Dkt. John Magufuli ameahidi moja ya vipaumbele vyake ni kushughulikia kero kubwa ya upatikanaji wa maji, ndio maana yeye na wataalamu hao wa Ruwasa na Dawasa wanatembelea wanakagua miradi hiyo ili kujionea inavyoendelea.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...